Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Nilikuwa ninatembea kama sehemu ya mazoezi ya asubuhi, nilikutana na mama mmoja umri waka utakuwa 50+. Tulisalimiana na alinieleza kuwa haamini kuwa ametembea mwendo wa mrefu vile. Aliniekeza kuwa miezi sita iliyopita hakuweza mwendo ule kwani ndiyo alikuwa anamalizia vita na cancer.
Kwa kweli nilikuwa ninahamu ya kusikiliza zaidi kwani wengi ninaokutana nao katika vita hii hakuna niliyekutana nae baada ya vita. Wengi hawafikii kutoa ushuhuda, lakini kwa mara ya kwanza nimekutana na mtu aliyepewa all clear “touch the wood”.
Nilimuomba mama huyu anieleze zaidi. Aliniambia alihisi uvimbe kwenye ziwa. Haraka waliwahi hospitali na alifanyiwa biopsy. Majibu yalithibitisha malignant.
Alifanyiwa upasuaji na ziwa lake kutolewa. Aliwekewa ziwa la plastic. Safari ya chemotherapy ilianza. Ilikuwa ni kila baada ya wiki tatu mwanzo wa matibabu baadae ilikuwa kila baada ya wiki tano.
Alisema chemo ni sumu halisi. Baada ya session mwili unabaki na nguvu ya kupumua tu, pale unapoanza kupata nafuu ni muda wa doze nyingine.
Ana watoto wanne binti mmoja na wakiume watatu. Binti ameolewa na ana watoto wadogo. Wa kiume mmoja alishahama nyumbani. Lakini habari zilipowafikia yule wa kiume aliyehama alirudi na alisaidiana na wadogo zake pamoja na baba yao kuuguza.
Hospitali walipeana zamu kumpeleka na watoto wote walijifunza kupika. Kabla ya hapo mama ndiye alikuwa mpishi mkuu wa familia.
Mwisho alisema safari hii imemfanya amjue Mungu na kuwa karibu nae sana. Yuko tayari kuongea na wagonjwa na wa cancer na kuwaeleza kuwa ni safari ndefu na ngumu lakini kuna matumaini siku hizi.
Ninakumbuka zamani kidogo nilikuwa kwenye clinic na daktari bingwa aliyetoa majibu ya biopsy kwa wagonjwa. Baba mmoja alifika na mkewe na walipopokea majibu mke alianza kulia. Yule baba aliitikia tu sawa, nilipojua kuwa yule mgonjwa hakuwa pale kimawazo na itamchukua muda kuelewa ni pale mke alipoulizia safari ya matibabu.
Ni muhimu kuambatana na mtu unaemuamini siju ya kuchukua majibu.