Nimekutana na mtu aliyeishinda Saratani

Nimekutana na mtu aliyeishinda Saratani

Nilikuwa ninatembea kama sehemu ya mazoezi ya asubuhi, nilikutana na mama mmoja umri waka utakuwa 50+. Tulisalimiana na alinieleza kuwa haamini kuwa ametembea mwendo wa mrefu vile. Aliniekeza kuwa miezi sita iliyopita hakuweza mwendo ule kwani ndiyo alikuwa anamalizia vita na cancer.

Kwa kweli nilikuwa ninahamu ya kusikiliza zaidi kwani wengi ninaokutana nao katika vita hii hakuna niliyekutana nae baada ya vita. Wengi hawafikii kutoa ushuhuda, lakini kwa mara ya kwanza nimekutana na mtu aliyepewa all clear “touch the wood”.

Nilimuomba mama huyu anieleze zaidi. Aliniambia alihisi uvimbe kwenye ziwa. Haraka waliwahi hospitali na alifanyiwa biopsy. Majibu yalithibitisha malignant.

Alifanyiwa upasuaji na ziwa lake kutolewa. Aliwekewa ziwa la plastic. Safari ya chemotherapy ilianza. Ilikuwa ni kila baada ya wiki tatu mwanzo wa matibabu baadae ilikuwa kila baada ya wiki tano.

Alisema chemo ni sumu halisi. Baada ya session mwili unabaki na nguvu ya kupumua tu, pale unapoanza kupata nafuu ni muda wa doze nyingine.

Ana watoto wanne binti mmoja na wakiume watatu. Binti ameolewa na ana watoto wadogo. Wa kiume mmoja alishahama nyumbani. Lakini habari zilipowafikia yule wa kiume aliyehama alirudi na alisaidiana na wadogo zake pamoja na baba yao kuuguza.

Hospitali walipeana zamu kumpeleka na watoto wote walijifunza kupika. Kabla ya hapo mama ndiye alikuwa mpishi mkuu wa familia.
Mwisho alisema safari hii imemfanya amjue Mungu na kuwa karibu nae sana. Yuko tayari kuongea na wagonjwa na wa cancer na kuwaeleza kuwa ni safari ndefu na ngumu lakini kuna matumaini siku hizi.

Ninakumbuka zamani kidogo nilikuwa kwenye clinic na daktari bingwa aliyetoa majibu ya biopsy kwa wagonjwa. Baba mmoja alifika na mkewe na walipopokea majibu mke alianza kulia. Yule baba aliitikia tu sawa, nilipojua kuwa yule magonjwa hakuwa pale kimawazo na itamchukua muda kuelewa ni pale mke alipoulizia safari ya matibabu.

Ni muhimu kuambatana na mtu unaemuamini siju ya kuchukua majibu.
Hakuna ugonjwa usio na dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kula healthy ni vizuri ili kuepuka haya magonjwa.

Lakini kula mboga ambazo hujui zilipuliziwa dawa lini, mimi naona ni risky.

Bora kupanda mboga zako kama una eneo ili uwe na uhakika unakula healthy food.

Lakini pia, kupunguza vyakula vya viwandani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Tena mboga mboga ni hatari sana aisee, mi hupanda mwenyewe kwenye ndoo zinakuwa Fresh nazinyeshea kuliko hizi mboga za huku Dar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The Disease and it's cure dwels in your mind,huwezi Amini kuna watu wamepona magonjwa yao just kwa kubadili fikra zao zao tu kuwa ugonjwa huu umenipata lakini si nwisho wa kuishi,wapo walio pona kabisa,hawa tunaowasikia wengine wanaanzisha mbio za marathon za kuchangia wahanga Fulani mfano wa relay for cancer wengi ni watu waliokuwa na hayo magonjwa na waliamini kuwa kuumwa si nwisho wa uhai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I agree. Lakini pia dawa za kienyeji zinafanya kazi.

Mama yangu alikuwa diagonised na cervical cancer. Kuna mtu akamwambia aende kwa baba mmoja hivi akapate matibabu. Huyo baba amesajiliwa kabisa na wizara ya afya. Nilimwambia mama hayo ni mambo ya kiganga achana nayo, nikamuomba tuzidishe maombi.

Mama alinijibu kujaribu sio mbaya. Hapa ninapozungumza mama yupo cancer free. Baada ya yale matibabu, vipimo vilionyesha hana cancer.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sir With Love, thanks for sharing such testimony. Hopefully our Mama is now healthy and well.

Nina mama yangu mdogo huko kijijini amekuwa diagnosed with cervical cancer. Hajanipa full clues, ila she just hinted that to me on phone convo. Nitampigia leo jioni then I will revert to you for further touches on possibilities ya kupata hiyo tiba uliyoisema.

Cancer ... cancer... cancer... the situation is now getting worse ktk jamii. The alarm is now alerting!! HELL ON EARTH.

-Kaveli-
 
I agree. Lakini pia dawa za kienyeji zinafanya kazi.

Mama yangu alikuwa diagonised na cervical cancer. Kuna mtu akamwambia aende kwa baba mmoja hivi akapate matibabu. Huyo baba amesajiliwa kabisa na wizara ya afya. Nilimwambia mama hayo ni mambo ya kiganga achana nayo, nikamuomba tuzidishe maombi.

Mama alinijibu kujaribu sio mbaya. Hapa ninapozungumza mama yupo cancer free. Baada ya yale matibabu, vipimo vilionyesha hana cancer.



Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani Kuna ushirikina na.uganga

Uganga unatumia dawa za mitishamba
Zinafanya kazi, sijui kwa nini hazikuzwi

[emoji252] [emoji479]
 
There is a beautiful healing prayer I came across, it says “Lord you created me from nothing and as I belong to you, you can recreate me again without any illness if it’s your will”.
"If it's God's will!!" Mara nyingi tunashindwa kuomba hii sala "Mapenzi ya Mungu yatimie". Hii ni zaidi ya kuomba uponyaji TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom