Nimekutana na mwanamke wa ajabu jioni ya leo. Jina la Bwana lihimidiwe

Nimekutana na mwanamke wa ajabu jioni ya leo. Jina la Bwana lihimidiwe

Ukiona vyaelea ujue vimeundwa bila kusahau starehe ni gharama.
Na kweli mkuu, miuno feni anayonipatia inasababisha kiasi kikubwa sana cha pesa kuishia kwake. Hana moyo wa shukurani, kuna siku atakutana na kitu kizito kichwani
 
Uzi mrefu ila in summary unataka kulelewa.
Hapana mkuu, nitalelewaje ilihali namiliki wake wawili na watoto? Kama alitaka nimuhudumie kwa kila hatua ya maisha yake, hakupaswa kufanya biashara kwa mtaji wangu, au kuniomba pesa ya maboresho ya biashara yake. Sasa kama pesa ya sukari ya mama yake ni juu yangu, yeye pesa anapeleka wapi?
 
Hapana mkuu, nitalelewaje ilihali namiliki wake wawili na watoto? Kama alitaka nimuhudumie kwa kila hatua ya maisha yake, hakupaswa kufanya biashara kwa mtaji wangu, au kuniomba pesa ya maboresho ya biashara yake. Sasa kama pesa ya sukari ya mama yake ni juu yangu, yeye pesa anapeleka wapi?
Mkuu umeielewa kweli comment yangu?
 
Sijaona shida yake hapo naunakula papuchi
Ni kwa vile sioni matunda ya biashara yake. Basi, ajitahidi ahudumie kwao sasa. Kila kitu mimi tu, tutafika kweli!!! Kisa miuno feni na maufundi ya Tanga na Zenji. Hapana kwa kweli
 
Mkuu umeielewa kweli comment yangu?
Ahaa! Kwamba atokee mwanaume mwingine wa kumhudumia? Haina shida, kikubwa anitimizie haja zangu na apunguze kuegemea kwangu katika kila jambo. Kingine nisijue kuwa yuko kwenye mahusiano na mtu fulani

Wanawake hawana dogo, huenda anajenga, huwezi jua.
 
Kheri yako dini inaruhusu kuongeza ,, ila muone huruma kijana denis wacha nae ufaidi raha duniani
 
kheri yako dini inaruhusu kuongeza ,, ila muone huruma kijana denis wacha nae ufaidi raha duniani
Kijana akiwa serious ni lazima atafaidi mema ya nchi. Tokea nimeyafahamu mapenzi, mwanamke wa namna huyo ndo namshuhudia kwa mara ya kwanza
 
Ni kwa vile sioni matunda ya biashara yake. Basi, ajitahidi ahudumie kwao sasa. Kila kitu mimi tu, tutafika kweli!!! Kisa miuno feni na maufundi ya Tanga na Zenji. Hapana kwa kweli
Achàna naye kaa na wake zako wawili nakabla hujaachana naye mwambie ukweli ila kama hutaki basi ila wewe unahitaji maombi unamatatizo kwenye ngono wake wawili na mchepuko Tena ???😆😆😆😝💔
 
Mbali na kuwa kwenye ndoa ya wake wawili waaminifu, nina mchepuko wangu anayeishi mtaa fulani. Mchepuko huyu nilimpatia mtaji, kwa kuwa yuko na akili ya maisha, alifanikiwa kufungua biashara na kuiendesha yeye kama yeye, biashara yenyewe ni ya uuzaji wa mboga i.e nyama za ndege, yaani kuku na bata

Mbali na kuwa na biashara yake inayompatia mamilioni ya pesa kwa siku, mchepuko huyu hana moyo wa huruma, kila siku huniomba pesa ya meza kana kwamba huwa ninakula kwake kila siku. Naumia sana ila najikaza kisabuni. Kuna muda mchepuko huyu hudiliki kuniomba pesa ya kujinunulia nguo au pedi, hapo ndipo huwa natamani kukipangua kibanda chake kwa mateke ya hapa na pale maake naona hakina msaada naye. Kuna siku nilitamani kumuwasha mbata hadharani pale aliponiambia eti tumtumie mama yake pesa ya sukari. Sasa biashara yake inamsaidia nini? Kwani mimi ni mumewe?

Mida ya saa kumi na mbili leo hii, amekuja binti mmoja mzuri na wa kuvutia, umbo lake lilifanana na chupa ya soda ya cocacola lililofunikwa na ngozi swaafi ya mzeituni, mkono wake wa kushoto uliushikilia mkono wa kuume wa kijana mmoja wa kufanana naye, nilidhani nimetembelewa na malaika wasio na mabawa

Basi bwana, nikaamua kuwalaki. Binti alikuwa si haba akaamua kuulizia bei ya nyama hizo, nikawa nimemtajia elfu tatu kwa elfu saba. Baada ya kushauriana, binti akaniomba nimfungie mboga ya 10k, muda huo yule kijana alikuwa akibubujikwa kijasho chembamba kuuzunguka mwili wake kuashiria hali ngumu ya maisha huku macho yake yakionesha wazi kuomba kikombe hicho kimuepuke

Kijana yule wa kiume ndipo kuniuliza totali ya mboga ile, baada ya kumwambia 10k aliingia kwa wallet na kuchomoa 10k iliyochakaa huku akiacha vumbi tu kwenye wallet ile. Binti alimuangalia kijana yule kwa huruma sana kisha kumwambia, "Usiwaze Denis, acha tu ntalipa". Mimi na Denis bila kumsahau mchepuko wangu tulipigwa na butwaa, ila mimi nilipigwa na butwaa kubwa kuwazidi wote huku nikiutazama ule mchepuko na kutikisa kichwa mithili ya mganga wa Yoruba kumwelekezea mchepuko kumaanisha kuwa mchepuko wangu ni kichwa box tupu la mbao

Niliipokea ile hela ya binti kwa heshima kubwa na taazima huku nikisindikizwa na mizinga mizito kutoka moyoni huku nikitoa matamshi ya kumchoma mchepuko wangu. Sauti ya Denis iliyonena, " Acha tu mpenzi, nitalipa mwenyewe tu" ilitaradadi kwa huruma ya hali ya juu pasi na kusikilizwa

Nilibaki nikimtazama binti akiwa anaishiria kuelekea kusikojulikana huku nikimuomba Mola anijaalie binti kama huyo ili awe mke wa tatu, au anipatie huyo huyo kama ikiwezekana

Ndipo kumuaga mchepuko huyo na kurejea nyumbani. Muda huu nipo kwa mke mdogo, tayari nimekwisha oga, nasubiri kuichapa baada ya makala kwa runinga
Utaoa dunia huyo nae ana yake mapungufu.
 
Back
Top Bottom