Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

KUKUSHAURI ILI ASIKUFATE TENA USIKU UNAPOLALA UJIPAKE MAFUTA YA NDIMU NA UWEKE KITUNGUU SWAUMU CHINI YA MTO HAJI TENA MAANA KHARUFU ZA MAFUTA YA NDIMU NA VITUNGUU SWAUMU VINAWAKERA SANA NA MAFUTA YA NDIMU HAKIKISHA UNAPAKA KILA MARA JAPO CHINI YA MAKWAPA ATAKIMBIA MWENYEWE
 
Habar zenu wadau. Naomba mnisaidie maana nipo njia panda sielew nifanye Nini.
Waswahili wanasema mficha maradhi Kifo humuumbua.
Mimi sitaki kusubiri Kifo kinikute. Ileweke nimekuwa humu JF kwa muda mrefu, Mara nyingi nimekuwa msomaji tu, wa matukio ya watu, pamoja na kujielimisha, Mara chache sana nimekuwa nikichangia mijadala pale inapobidi. Hii ndio thread yangu ya kwanza. Hivyo sijaandika kwa ajili ya kuburudisha/kumtisha mtu, ninachokiwasilisha hapa Ni ukweli mtupu. Lengo na madhumuni Ni kupata ushauri na msaada pale inapobidi.

***** ****** ******** ******** ******
Iko hv, Mimi Ni mfanya biashara mdogo ninaejishughulisha na uuzaji wa nguo za kiume katika sehemu Fulani hv hp jijini DSM. Kiufupi Nina maduka mawili ya nguo za kiume, hiyo ndio ajira yangu inayonifanya niishi hapa mjini. Sasa mnamo Tar 27 Dec ya mwaka Jana (2018)nipo ktk moja ya ofisi yangu na endelea na majukumu yangu ya kawaida, tena nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi mida ya Kama saa 7 mchana kuelekea saa 8 hv, alikuwa mteja ambae Ni mwanamke ( Alikuwa mrembo sana, mweupe Ana asili Kama ya kiarabu hv) ila rafudhi Ni yakipemba. Kama kawaida nikawa namsikiliza, akaniambia nimchagulie nguo nzuri anataka ampelekee mme wake, Yani shati na suruali.
Wakati naendelea kumchagulia nikawa namuuliza anavaa size gani? Akacheka akasema yupo Kama wewe, kwa kila kitu...Tena akaongeza na kusema nguo nitakazo zipenda Mimi hata yy atazipenda.
Nikawa namtania, nikamwambia kwa jinsi ulivyomzur hvy nataman mume wako niwe Mimi, akaniuliza Kweli? Nikamwambia hakuna mwanaume chini ya jua anaweza kukukataa msichana mrembo Kama wote tukacheka.
Zoezi la kuchagua nguo likaendelea tukafanikiwa kupata nzuri akazipenda. Tumezoea wabongo tunapenda discount, lkn kwake ilikuwa ni tofauti, akauliza nikiasi gani alipe, nikamwambia akalipia bila kuomba punguzo la Bei Kama tulivyozoea kwa wateja walio wengi. Wateja wa namna hii hutokea ila ni marachache sana, hvy nilifurah maana inakuwaga bingo unapata faida nzur.
Nikiwa namfungia hz nguo, aliniuliza...umeoa? Nikamwambia hapana akacheka akasema, nilijua tu...huwez kuoa mapema 7bu unapenda pombe na wanawake wa aina tofauti tofauti, kifupi we Ni mzinifu. Hii ya pombe ilinistua kidogo, amejuaje mm nakunywa pombe, ila sikutaka kumuonesha hadharani.
Akaniambia, Kuna sehemu anaenda hvy akirudi atauputia mzigo wake, ila nimuhifadhie, akaniuliza huwa nafunga saa ngapi? Nikamwambia, akaniomba namba ya simu Kama sitojali nimpe ili Kama atachelewa anijulishe nisije chelewa kufunga kwa 7bu yake. Nami sikuona Tatizo, kwanza Ni mteja lakini pia Ni mrembo sana[emoji847] Kama tunavyojijua sisi wanaume, basi nikampa namba, akaaga na kuondoka.
************
Hapo ndipo kizazaa kilipoanza. Hata hapa naandika thread hii, Sina amani kabisa. Kufika mida ya Kama saa mbili na robo usiku, sms ikaingia kwenye simu yangu.inasema "Zawadi niliyo kununulia umeipenda"? Mmmh, mm nikahisi itakuwa mtu kakosea namba, coz ilitokea namba mpya, baada ya Kama dk 10 hv, ile namba iliyotuma sms ikawa inanipigia, kupokea nasikia sauti ya msichana, akaniuliza...mbona hujajibu sms yangu hau unapenda zawadi yangu, nikamuuliza unajua unaongea na Nan?
Akasema ndio Ni Fulani (akataja jina langu), nikashangaa nikamwambia mbona hakuna mtu nilimwagiza zawadi akasema, Tena umechagua na kuzijaribisha mwenyewe Mara hii umesahau? [emoji849][emoji50] Akawa anacheka[emoji1787][emoji1787][emoji1787] akaniuliza umeshanikumbuka? Nikamwambia ndio...nikamuuliza umejuaje jina langu wakati sikumtajia, (Nilimdanganya jina) Mara nyingi Sina destruri ya kukwambia jina langu la ukweli mtu nisie mjua, Hilo likanishangaza...nikachekecha akili nikahis labda ameangalia kwenye tigo pesa maana nilimpa namba ya tigo, swali lililozidi kuniumiza akili anawezaje kuja dukani kwangu kuninulia nguo Ikiwa hanifahamu, wakat aliniambia Ni za mumewe?
Nikamuuliza si ulisema unampelekea mumeo? Akaniambia kwani wewe hufai kuwa mume wangu? Akiwa anacheka, akaendelea.....na si ulisema hujaoa au ulinidanganya? Nikabaki na kigugumiz nisiamini ninachokisikia, akaniambia nimeamua kukutunuku. Usiku mwema, nitakuja kukutembelea siku nyingine akakata simu. Nikabaki na maswali chungu nzima, kupiga ile namba ikawa haipatikan...baada ya hapo ndio vitimbi vilipoanza.

Itaendelea.......

NB: Nimechoka kuandika nitaendelea kesho ila kiukweli mwezenu nipo njia panda sielew, mwaka nimeanza na mauzauza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni pm namba yake huyo nimfundishe adabu [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah pole kubwa sana mkuu. Kama ni Muislam wapo masheikh wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hayo masuala kwa dua nzito tu. Na kwa hayo masuala usithubutu kwenda kwa Waganga wa Kienyeji. Hivyo vitu na masuala ya kienyeji ni mbalimbali kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mawili.

Mleta Uzi ni mfanyabiashara na wafanyabiashara huwa wanafahamika zaidi kwa watu kuliko wao wanavyofahamiana na watu.

Mosi: Aondoe hofu kwanza inawezekana ni binadamu tu na mwanaume kupendwa na mwanamke si ajabu, na si ajabu mfanyabiashara kufahamika zaidi. Pengine huyo binti anamfahamu huyu jamaa na ametokea kuvutiwa naye. Tunafahamu ulevi wa mapenzi unakuaje, pengine huyo binti ametumia hiyo njia ili iwe mwanzo wa mahusiano yao.

Pili: Kama uhalisiya ni sawa sawa na hisiya zake, wadau wengi wamemshauri ni nini cha kufanya. Nina imani atafanikiwa vya kutosha. Pasipo kusaha jambo ulilomshauri ni jambo jema la kutojishughulisha kwa waganga wa kienyeji kwa kadhia yake.
 
Iliwahi kunitokea saa nane usiku nimelala usingizi mzito Pazia la dirisha sikulishusha ila vioo Nimefunga sasa nikazinduka ghafla usiku nikakuta jamaa ananiangalia kwa utulivu na hata alipojua nimemuona hakuondoka nilipopiga kelele hakuondoka nikaduwaa siamini baada ya dk tatu akaondoka mwenyewe
Dah we jamaa umenifanya nicheke saan yaan saan

Dah ulipiga kelele za kuashiria nin?mwizi au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mawili.

Mleta Uzi ni mfanyabiashara na wafanyabiashara huwa wanafahamika zaidi kwa watu kuliko wao wanavyofahamiana na watu.

Mosi: Aondoe hofu kwanza inawezekana ni binadamu tu na mwanaume kupendwa na mwanamke si ajabu, na si ajabu mfanyabiashara kufahamika zaidi. Pengine huyo binti anamfahamu huyu jamaa na ametokea kuvutiwa naye. Tunafahamu ulevi wa mapenzi unakuaje, pengine huyo binti ametumia hiyo njia ili iwe mwanzo wa mahusiano yao.

Pili: Kama uhalisiya ni sawa sawa na hisiya zake, wadau wengi wamemshauri ni nini cha kufanya. Nina imani atafanikiwa vya kutosha. Pasipo kusaha jambo ulilomshauri ni jambo jema la kutojishughulisha kwa waganga wa kienyeji kwa kadhia yake.
Uko sahihi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya hii iwe fundisho kwenu wanaume mnaokurupukia wasichana wazuri
Huyajui majini mahaba wewe, hata usipokua mtongozaji likishakupenda lazima likufatilie tu. Kiboko yake ni maombi ya kutosha hakuna kingine
 
Habar za muda wanajamvi. Soon nawawekea Nini kilichojiri. Ila naomba kutoa angalizo na Rai, kwa baadhi ya wachangiaji humu. Mimi sio mtunzi Kama wengi mnavyodhani, hiki ninachokileta mbele yenu, Ni wakat ambao napitia Sasa...nipo wakat mgumu sana. Hv ninavyoandika, nimetawaliwa na hofu na wasiwasi mkubwa, nahitaj msaada wenu. Niombeeni tafadhali mtihani niupitiao Ni mzito sana. Na mnaokuja PM, Kama Huna lengo la kunishauri ni vyema ukaacha kuliko kuendelea kunitisha kwamba nitakuwa pamoja na kunidhiahak, ama Kweli binadamu hatufanani, sikutegemea Kuna watu watanibeza na kuniogopesha kiasi hiki badala ya kunisaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya MKUU fanya umalizie tujue namna ya kukushauri basi!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati tuko high school kuna dada alishakutana na hao viumbe. Aliishi kwa shida sana shule. Alikua akipandisha maruhani yake utamuonea huruma. Sijui kama aliponaga maana mpaka tunamaliza form six alikua bado anazunguka kwa wachungaji amfukuze mume wake wa ujinini.
Kilichomponza alipewa Pete na huyu dada wa jini akajua Pete kweli kumbe ilikua Pete yake ya ndoa na huyo jini. Na mtoto walikua nae

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka gani huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom