Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Hapa umecheza fresh. Watu watakuja kuomba namba ya huyo mlinzi.wewe utawaunganisha na jamaa ambaye tayari mpo naye kwenye mchakato.halafu unakula cha udalali.

 
Humu watakuja watu kuyatete majini na uzi utaishia kuwa vita vya kidini.watu upande wa majini na walio kinyume na majini. Subirini tu.
 
Unamwelekeza ushirikina halafu unamwambia alale na biblia unadhani biblia inamzuia shetani?shetani naye anaijua biblia na anaisoma sana tu.hayo ya kuoga maji chumv na kunuiza tayari ni ushirikina.usichanganye madesa

 
Jamani eeeh samahani sana kwa kupachika swali nje ya mada,

Ni kwamba pm yangu inaonyesha kuna SMS tatu,lakini nikifungua inaniambia empty msg hii naitatuaje niweze kusoma SMS zangu!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amkabidhi Yesu maisha yake, halafu kila siku ale nguruwe. Jini na nguruwe ni maji na moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wanajamvi, kipekee kabisa nipende kuwashukuru, kwa michango yenu katika ushauri juu ya tatizo lililo nikumba. Pia, namshukuru Mungu naendelea vyema kabisa, ingawaje vita ni kubwa mno...kwa sasa nimeshauriwa nisiseme chochote (sio kwa ubaya) ila ni kwa ajili ya usalama wangu pia.

Kwa wale wenye hofu na wasiwasi mm ni mzima wa afya... Ingawaje kumetokea mambo mengi sana ya kunirudisha nyuma, ikiwa ni pamoja na matapeli waliochukulia tatizo langu kama fursa. Nimepoteza pesa nyingi sana katika kutafuta suluhu la jambo langu, lakini nikiri wazi Mungu aliejuu mbinguni ashindwi na kitu, naamii atarejesha kila nilichopoteza.

Kwa sasa nimefunga biashara zangu zote (kwa muda) ili niokoe maisha yangu. Kwa sasa nipo kambini na timu ya maombi sehemu fulani (nisingependa kupataja) wananifanyia huduma. Kiukweli kabisa Vita ni kubwa mno Mama yangu kaponea chupu chupu kumpoteza.

Pia niwaweke wazi katika hili...mimi ndio msaada mkubwa katika familia yangu, matatizo haya yamesababisha ni yumbe sana kiuchumi. Hapa nilipo sina chochote (fedha) timu ya maombi inakesha usiku na mchana kunipigania..ukweli ni kwamba kama si nyinyi wana JF kunisisitiza ishu ya maombi nisingekuwa hai sasa. Naomba muendelee kuniombea pia.

Nashindwa nisemeje lkn najisikia aibu na fedhea kubwa kwa watu wanaopigania maisha yangu kushindwa kuwahudumia hata chakula na maji. Sio malipo kama wengine walivyohitaji ni bure kabisa ila hawa nao pia ni binadamu. Kama kuna yoyote ataguswa katika hili naomba aje Pm nitampa utaratibu aweze kunichagia chochote alichonacho (Nisieleweke vibaya tafadhali) kama utaguswa katika hilo naamini kabisa Mungu hatukuacha kama ulivyo ulipotoa atakuongezea mara dufu.

Nawashukuru sana kwa msaada wenu wana Jamii Forum. Niwatakie mchana mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kwa kuchangamkia fursa. Nawe umeona uje utangaze biashara yako huku? Kweli JF kiboko. Wanawake wenye akili huwa hawapendi kabisa wajulikane au waonekane hata kidole.wewe unatuwekea picha za ngwala zako ili watu waanze kukutafuta ?maana nyie ndo mnaitwa mizoga mnawatega mafisi ambayo anytime yanataka kula wanawake mizoga.

Mnataka kuharinu uzi wa jamaa hapa kwa nini msitumiane pembeni mpaka uje kufanya matangazo kwenye uzi wa watu?


 
Wewe muongo ungeendelea kutupa hii stories si lazima uifanye iwe kama ya kweli.unakuja hapa eti umetapeliwa n.k na umeshauriwa usiandike....au aliyekuwa anaandika sehemu uliyokuwa una copy ameacha?amekushtukia?

Hivi ni lazima kila ukiandika story useme ni ya kweli?sisi wengine tukiwa free tunasoma tu wala si shida si lazima mpaka useme imekutokea.au ulitaka baadaye uaje uanzishe biashara flan hapa.....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…