Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Habari zenu wanajamvi, kipekee kabisa nipende kuwashukuru, kwa michango yenu katika ushauri juu ya tatizo lililo nikumba. Pia, namshukuru Mungu naendelea vyema kabisa, ingawaje vita ni kubwa mno...kwa sasa nimeshauriwa nisiseme chochote (sio kwa ubaya) ila ni kwa ajili ya usalama wangu pia.

Kwa wale wenye hofu na wasiwasi mm ni mzima wa afya... Ingawaje kumetokea mambo mengi sana ya kunirudisha nyuma, ikiwa ni pamoja na matapeli waliochukulia tatizo langu kama fursa. Nimepoteza pesa nyingi sana katika kutafuta suluhu la jambo langu, lakini nikiri wazi Mungu aliejuu mbinguni ashindwi na kitu, naamii atarejesha kila nilichopoteza.

Kwa sasa nimefunga biashara zangu zote (kwa muda) ili niokoe maisha yangu. Kwa sasa nipo kambini na timu ya maombi sehemu fulani (nisingependa kupataja) wananifanyia huduma. Kiukweli kabisa Vita ni kubwa mno Mama yangu kaponea chupu chupu kumpoteza.

Pia niwaweke wazi katika hili...mimi ndio msaada mkubwa katika familia yangu, matatizo haya yamesababisha ni yumbe sana kiuchumi. Hapa nilipo sina chochote (fedha) timu ya maombi inakesha usiku na mchana kunipigania..ukweli ni kwamba kama si nyinyi wana JF kunisisitiza ishu ya maombi nisingekuwa hai sasa. Naomba muendelee kuniombea pia.

Nashindwa nisemeje lkn najisikia aibu na fedhea kubwa kwa watu wanaopigania maisha yangu kushindwa kuwahudumia hata chakula na maji. Sio malipo kama wengine walivyohitaji ni bure kabisa ila hawa nao pia ni binadamu. Kama kuna yoyote ataguswa katika hili naomba aje Pm nitampa utaratibu aweze kunichagia chochote alichonacho (Nisieleweke vibaya tafadhali) kama utaguswa katika hilo naamini kabisa Mungu hatukuacha kama ulivyo ulipotoa atakuongezea mara dufu.

Nawashukuru sana kwa msaada wenu wana Jamii Forum. Niwatakie mchana mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
mtiririko wa story yako.ni well arranged,ila umekuja kuharibu hapo pa kutaka michango tu...hahahahaaaa umefanya nianze kutokukuamini ingawa mambo haya yapo na mimi mwenyewe ni shuhuda kwa mtoto wa shangazi yangu...long story but alipona kwa maombi ya nguvu bila kuomba mchango wa pesa kwa mtu yoyote yule
 
Mmmh GuDume kaandika kuhusu wewe dakk 5 hazijapita wewe umekuja na Uzi wa kuomba msaada.
Jee kuna uhusiano wa hii I'd na gudume? Kwa nini aandike na wewe ndiyo uje na huu Uzi?
Je ni gudume anafanya hivi ili kutuonyesha anajua kutabiri? Yote yanawezekana.
Suspect everything, trust nothing.[emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
wapi uko mkuu?
 
Dereva wa baba yangu alifanyiwa maombi mwaka Mzima kila kona unayoijua wewe, mwisho wa siku kaaga dunia. Alikuwa dereva kwa miaka 8 lakini alikuwa kama ndugu kwakweli, nikirudi kwako mkuu. Duka unalo kwanini usimuweke ndugu yako dukani? Halafu ukalifanyia maombi hilo duka lako pia. Mtu chake kwanini usiuze hio gari yako na kukusaidia kwa sasa, huoni aibu kuomba? Unasema watu wamekutapeli kwa kuona matatizo yako fursa ya kufanya utapeli. Kwanini na sisi tusihisi kama umetumia stori yako kuja kututapeli?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
January mbaya sana hiii daadeki wakikuchangia niambie shubaamiti.
Wenye moyo na ubinadamu wanajua shida nini...Mungu ambariki Alphonce kwa alichotoa sio haba, Tsh2000/= naamini sio kwamba alikuwa nacho sana ila lahasha ila anajua dunia duara. Pindi tu nilipoandika uzi wa kuomba mchango yy ndio amekuwa wa kwanza. Mungu akubariki sana Alphonce

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh GuDume kaandika kuhusu wewe dakk 5 hazijapita wewe umekuja na Uzi wa kuomba msaada.
Jee kuna uhusiano wa hii I'd na gudume? Kwa nini aandike na wewe ndiyo uje na huu Uzi?
Je ni gudume anafanya hivi ili kutuonyesha anajua kutabiri? Yote yanawezekana.
Suspect everything, trust nothing.[emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
Lolote linawezekana kwa yule kiumbe
 
It means alikuja kutafta Kiki hafu kilicho ni shangaza gudume kasema hao watu matapeli atakuja ajifanye Kuna member kamchangia kiasi flani na kumsifia. Na huyu mleta mada kasema Kuna mtu kashamchangia hii ni coincidence or what
Alileta Uzi wake wa kukandia wadada akaona amepata shavu sasa kaja na utabiri feki ili wazidi kumwamini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom