Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Pole sana mkuu, huyo ni mpenzi jini amekutunuku

Kuna tiba moja rahisi sana inaweza kukusaidia ukiifanya kwa bidii. Chumvi!!

Nenda kanunue chumvi ya mawe sokoni alafu uwe unaweka kwny maji yako ya kuoga (nusu kiganja cha mkono)

Oga fresh ukimaliza yale maji ya mwisho (ndo yatakuwa na chumvi haswa) jimwagie na mikono kama unaoga hv huku unanenea maneno ya kujisafisha na kujinasua kwa huyo jini kisirani.

Nuia kila kitu, kama umelishwa vitu vichafu nuia vitoke, kama umechanjwa futa kama umetupiwa nuia litoke. Fanya hvyo kila siku asbh na jioni kwa siku saba, hatakusumbua tena huyo kibwengo.

Pendelea kulala na biblia kitandani

Pendelea kulala redio ikiwa on weka station za dini hasa praise power.

Mungu akuvushe salama katika janga hilo. Ila amini litaisha na utakuwa salama tu

Be Humble is free of charge [emoji873]
Na wewee umechanganya uchawi na bibilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe muda wote unalialia tu niko kwenye wakati mgumu,wakati mgumu. Mimi sijaona jini alipokuweka kwenye wakati mgumu au mazingira hatarishi,ila ni wewe mwenyewe unajihatarishia. Kuna shida gani wewe ukiolewa na jini? Hakuna mahala amekufanyia vibaya,wala kukutukana,ila wewe unamtukana. Kweli cha moto unaweza ukakiona ksbb unamtukana,kama kumchokoza. Mshana (nafikiri) slishawahi kuna majini wazuri na wabaya. Huyo jini mzuri kabisa huyo,unamuogopa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Bwana wewe jini ni jini tu hakuna cha jini mbaya wala jini mzuri, sasa huyu anayetumia mamlaka yake ya giza kulazimisha mahusiano ndio utasema mzuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, huyo ni mpenzi jini amekutunuku

Kuna tiba moja rahisi sana inaweza kukusaidia ukiifanya kwa bidii. Chumvi!!

Nenda kanunue chumvi ya mawe sokoni alafu uwe unaweka kwny maji yako ya kuoga (nusu kiganja cha mkono)

Oga fresh ukimaliza yale maji ya mwisho (ndo yatakuwa na chumvi haswa) jimwagie na mikono kama unaoga hv huku unanenea maneno ya kujisafisha na kujinasua kwa huyo jini kisirani.

Nuia kila kitu, kama umelishwa vitu vichafu nuia vitoke, kama umechanjwa futa kama umetupiwa nuia litoke. Fanya hvyo kila siku asbh na jioni kwa siku saba, hatakusumbua tena huyo kibwengo.

Pendelea kulala na biblia kitandani

Pendelea kulala redio ikiwa on weka station za dini hasa praise power.

Mungu akuvushe salama katika janga hilo. Ila amini litaisha na utakuwa salama tu

Be Humble is free of charge [emoji873]
Mwanzo umetoa maelezo kama mganga wa kienyeji baadae kama mtumishi haha ma mdogo umenishinda tabia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa imani yangu majini na wanadamu sote tumeumbwa na Allah,na hatutakiwi kuwa na muingiliano wowote sote kazi yetu ni kumuabudu yeye Muumba wetu.
Hapo sasa utaona hakuna jini mzuri kwa mwanadamu maana jini yoyote akishirikiana na wanadamu anakua ameshakengeuka,mwanzo atakuja kama mzuri kwako na huenda hata akakulazimisha kwenda kuswali lakini mwishoni ataanza kukupa masharti bila wewe kujua mfano ukaambiwa uvae pete ukiivua unapoteza bahati,kwa imani ya kiislam vyote vya mwanadamu vinatoka kwake Allah lolote la kuamini mfano pete,siku,muda,majini kua ndio either yatakuongezea kipato/uhai etc au yatakupunguzia huko ni kumshirikisha Muumba wako,naye hana mshiriki yoyote yule. Ni dhambi kubwa sana zaidi hata ya kuua na kuzini.
Amini jini hawezi kukufanya lolote yeye kama yeye lazima atumie watu maana yeye hana uwezo hata wa kukukaba angekua na uwezo huo wangetumaliza sana,majini hawana uwezo wa kujua lolote unalowaza moyoni wao wanaona lile unaloandika au lile unalolisema. Hivyo tumia udhaifu wao kupambana nao
Kwanza uwe msafi sio unaswali kwa kugusa gusa swali haswa na funga itakusaidia sana,pili mambo yako yaweke moyoni ikiwezekana unalosema lisiwe unalolifanya mfano unaweza ikawa baadae unaenda ibadani ila wewe unaweza mpigia rafiki yako kua aise naenda beach jioni,yeye ataenda kukusubiri beach wewe unaenda ibadani. Rudi kwa Muumba wako tena usifanye IBADA KWA KUBEEP FANYA IBADA KAMA INAVYOTAKIWA HASWA,teyari una mtihani sasa sio asubuhi ibadani jioni bar hautofanikiwa mkuu.Mwenyezi Mungu atakusaidia ila usimsikilize jini atakupotezea dunia na kesho akhera.
Namuomba Muumba akusaidie In Sha Allah
 
100% correct, nilifukuzwa kazi, gari yangu ikawaka moto nikiwa kwenye foleni, nilifilisika nikakosa hata mia wala kiatu cha kuvaa, hakuna rafiki, ndugu wala mwanafamilia aliyetaka.kuniona..nikawa nafikiria nisafiri niende mbaalii nisipo pajua (Technically kumbe mawazo ya kujiua).. Hawa viumbe washenzi sana wakiamua kukukomesha.
Sasa Kwa nn wanafanya ivi .ikiwa wanakupenda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah maisha mwanzoni yalikuwa km kawaida tu lkn baadae nikaanza kuporomoka kiuchumi,nikayumba sn then unabanwa kila kona unakosa kibali kwa kila mtu si ndugu,jamaa wala rafiki. Unakosa wa kukusapot then anakuchonganisha nao wote unabaki km bundi yaani ni balaa mwanzo mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Kwa nn wanafanya ivi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bangi bangi bangi usiivute mchana kweupee.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Bwana wewe jini ni jini tu hakuna cha jini mbaya wala jini mzuri, sasa huyu anayetumia mamlaka yake ya giza kulazimisha mahusiano ndio utasema mzuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu hakuna shetani mzuri. Yaani Kuna jamaa mwaka jana mwanzoni alifanyiwa kitu mbaya na mtu/jini/msukule sijui niuite jina gani. Huyo jamaa ni boda, inasemekana ana tabia ya kutoboa ozone (kukesha akitafuta faranga). Sasa majira fulani ya usiku mnene akapata kichwa Cha kike kinaulizia mahala pa kulala. Jamaa akamwelekeza mteja wake na wakakubaliana ampeleke kwa kuwa ni usiku. Kufika logde haifahamiki walianzia vipi mpaka wakakubaliana wafanye mchikicho. Kule ndani jamaa anasimulia baada ya round sijui ya tatu sikumbuki, akaulizwa na mteja wake, "ulikula?" Jamaa akakubali, swali la pili la mteja jini jike " kwa kawaida yako huwa unaenda mara ngapi mbona umechoka mi bado?" Sikumbuki jamaa alichosimulia kumjibu huyo malikia. Ila anasema alifanyiwa usodoma wa hatari na huyo msukule jini mpaka akachanika (maana damu zilimtoka akashindwa kutembea kiasi Cha kuhitaji msaada pale lodge). Wakati anatendewa hayo mambo alikuwa akishuhudia kwa ufahamu wake but uwezo na nguvu wa kukataa au kupiga kelele haukuwepo.

Alikuja kupata ufahamu tu baadae kumekucha jua jeupe baada ya hamaki kile kilichomkuta (hallucinating) na ambapo alilazimika kupiga kelele ili kupata msaada kwa wahudumu wa ile lodge. Na alipoulizia huyo mgeni wake aliyempeleka pale kama wamebahatika kumwona, ilionekana hawakuona mtu yeyote kutoka ndani ya ile lodge toka walipoingia.

Msidhanie haya mambo ni ya kudhani au kitu ya bumbuwazi au kitu ya hallucination.

"Anyway kusoma sana nako hupotosha"
 
Habar zenu wadau

Naomba mnisaidie maana nipo njia panda sielewi nifanye nini. Waswahili wanasema mficha maradhi Kifo humuumbua.

Mimi sitaki kusubiri Kifo kinikute. Ileweke nimekuwa humu JF kwa muda mrefu, Mara nyingi nimekuwa msomaji tu, wa matukio ya watu, pamoja na kujielimisha, Mara chache sana nimekuwa nikichangia mijadala pale inapobidi. Hii ndio thread yangu ya kwanza. Hivyo sijaandika kwa ajili ya kuburudisha/kumtisha mtu, ninachokiwasilisha hapa Ni ukweli mtupu. Lengo na madhumuni Ni kupata ushauri na msaada pale inapobidi.

***** ****** ******** ******** ******
Iko hv, Mimi Ni mfanya biashara mdogo ninaejishughulisha na uuzaji wa nguo za kiume katika sehemu Fulani hv hp jijini DSM. Kiufupi Nina maduka mawili ya nguo za kiume, hiyo ndio ajira yangu inayonifanya niishi hapa mjini. Sasa mnamo Tar 27 Dec ya mwaka Jana (2018)nipo ktk moja ya ofisi yangu na endelea na majukumu yangu ya kawaida, tena nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi mida ya Kama saa 7 mchana kuelekea saa 8 hv, alikuwa mteja ambae Ni mwanamke ( Alikuwa mrembo sana, mweupe Ana asili Kama ya kiarabu hv) ila rafudhi Ni yakipemba. Kama kawaida nikawa namsikiliza, akaniambia nimchagulie nguo nzuri anataka ampelekee mme wake, Yani shati na suruali.
Wakati naendelea kumchagulia nikawa namuuliza anavaa size gani? Akacheka akasema yupo Kama wewe, kwa kila kitu...Tena akaongeza na kusema nguo nitakazo zipenda Mimi hata yy atazipenda.
Nikawa namtania, nikamwambia kwa jinsi ulivyomzur hvy nataman mume wako niwe Mimi, akaniuliza Kweli? Nikamwambia hakuna mwanaume chini ya jua anaweza kukukataa msichana mrembo Kama wote tukacheka.
Zoezi la kuchagua nguo likaendelea tukafanikiwa kupata nzuri akazipenda. Tumezoea wabongo tunapenda discount, lkn kwake ilikuwa ni tofauti, akauliza nikiasi gani alipe, nikamwambia akalipia bila kuomba punguzo la Bei Kama tulivyozoea kwa wateja walio wengi. Wateja wa namna hii hutokea ila ni marachache sana, hvy nilifurah maana inakuwaga bingo unapata faida nzur.
Nikiwa namfungia hz nguo, aliniuliza...umeoa? Nikamwambia hapana akacheka akasema, nilijua tu...huwez kuoa mapema 7bu unapenda pombe na wanawake wa aina tofauti tofauti, kifupi we Ni mzinifu. Hii ya pombe ilinistua kidogo, amejuaje mm nakunywa pombe, ila sikutaka kumuonesha hadharani.
Akaniambia, Kuna sehemu anaenda hvy akirudi atauputia mzigo wake, ila nimuhifadhie, akaniuliza huwa nafunga saa ngapi? Nikamwambia, akaniomba namba ya simu Kama sitojali nimpe ili Kama atachelewa anijulishe nisije chelewa kufunga kwa 7bu yake. Nami sikuona Tatizo, kwanza Ni mteja lakini pia Ni mrembo sana[emoji847] Kama tunavyojijua sisi wanaume, basi nikampa namba, akaaga na kuondoka.
************
Hapo ndipo kizazaa kilipoanza. Hata hapa naandika thread hii, Sina amani kabisa. Kufika mida ya Kama saa mbili na robo usiku, sms ikaingia kwenye simu yangu.inasema "Zawadi niliyo kununulia umeipenda"? Mmmh, mm nikahisi itakuwa mtu kakosea namba, coz ilitokea namba mpya, baada ya Kama dk 10 hv, ile namba iliyotuma sms ikawa inanipigia, kupokea nasikia sauti ya msichana, akaniuliza...mbona hujajibu sms yangu hau unapenda zawadi yangu, nikamuuliza unajua unaongea na Nan?
Akasema ndio Ni Fulani (akataja jina langu), nikashangaa nikamwambia mbona hakuna mtu nilimwagiza zawadi akasema, Tena umechagua na kuzijaribisha mwenyewe Mara hii umesahau? [emoji849][emoji50] Akawa anacheka[emoji1787][emoji1787][emoji1787] akaniuliza umeshanikumbuka? Nikamwambia ndio...nikamuuliza umejuaje jina langu wakati sikumtajia, (Nilimdanganya jina) Mara nyingi Sina destruri ya kukwambia jina langu la ukweli mtu nisie mjua, Hilo likanishangaza...nikachekecha akili nikahis labda ameangalia kwenye tigo pesa maana nilimpa namba ya tigo, swali lililozidi kuniumiza akili anawezaje kuja dukani kwangu kuninulia nguo Ikiwa hanifahamu, wakat aliniambia Ni za mumewe?
Nikamuuliza si ulisema unampelekea mumeo? Akaniambia kwani wewe hufai kuwa mume wangu? Akiwa anacheka, akaendelea.....na si ulisema hujaoa au ulinidanganya? Nikabaki na kigugumiz nisiamini ninachokisikia, akaniambia nimeamua kukutunuku. Usiku mwema, nitakuja kukutembelea siku nyingine akakata simu. Nikabaki na maswali chungu nzima, kupiga ile namba ikawa haipatikan...baada ya hapo ndio vitimbi vilipoanza.

Itaendelea.......

NB: Nimechoka kuandika nitaendelea kesho ila kiukweli mwezenu nipo njia panda sielew, mwaka nimeanza na mauzauza

Sehemu ya Pili



Sehemu ya Tatu




Sent using Jamii Forums mobile app
Hasa
 
Huwa napata tabu kumuelewa kijana tena anaejitanabaisha kuwa wa kiume..

kwanza, akitumia emoji katika maandishi yake

Pili, kukatisha maneno eti '7bu'..sasa hako ndio kakitunguu swaumu gani?

Anyway..hapo njia panda unafanya nini saivi? Au ndio unakula mavitunguu swaumu ili uje uendelee?


Ni mwanamme wa Dar, kuwa mvumilivu tu...si unawajuwa desturi zao?
 
duuuuh mwamba pole xana ila msaaada mkubwa ni kanisani au msikitini kaombewe au wakufanyie dua
 
Back
Top Bottom