Nimekutana na mwanaume Kawe ananiambia ananifananisha

Nimekutana na mwanaume Kawe ananiambia ananifananisha

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Leo nilikuwa katika mizunguko yangu ya hapa na pale humu jijini Dar,katika kipindi hiki cha mapumziko

Lakini alasiri hii nikiwa duka moja huku kawe kuna wanaume wawili wamenifuata wakiniambia wananifananisha,wanaomba tufahamiane vizuri

Nikawambia mnahisi mmewahi kuniona wapi,wamedai Jf,nimewambia hamna mtakuwa mnanifananisha,nikaita Tax nikaondoka

Kumbe wanaume wa humu wako vizuri katika kumchunguza mtu
 
Wawili!! bora ulijiondokea.. wangeweza kukudhuru. Hata kama washakuona kabla humu
 
Kumbe hii Avater hapa ni wewe mwenyewe, umenisaidia kuelewa hilo kadada.
 
Leo nilikuwa katika mizunguko yangu ya hapa na pale humu jijini Dar,katika kipindi hiki cha mapumziko

Lakini alasiri hii nikiwa duka moja huku kawe kuna wanaume wawili wamenifuata wakiniambia wananifananisha,wanaomba tufahamiane vizuri

Nikawambia mnahisi mmewahi kuniona wapi,wamedai Jf,nimewambia hamna mtakuwa mnanifananisha,nikaita Tax nikaondoka

Kumbe wanaume wa humu wako vizuri katika kumchunguza mtu
Ndio wamekuchunguza na wamepatia kwamba kweli uko JF,lakini the bottomline is umewavutia.Dada tulioko JF pia ni watu.
 
Hapo kwenye avatar kama ni wewe; ngoja nije pm nami nikufananishe.
 
Una bahati sana wewe dada.
Tulitaka kukupeleke kusikojulikana ili tukuoe kabisa.

Joking
 
Hao matapeli tu walikua wanataka wakamilishe mpango
 
Safi sana...

Usingeondoka, ungewasikiliza...
kama unashinda MMU huna cha kuogopa, ila kama unashinda jukwaa la Siasa na watu wakakufuata na kusema wanakufafanisha wakatae kabisa...

Cc: mahondaw
 
Ukaita tax?...sidhani kama TRA wanahuduma za kuita tax.

Ulivyoita tax ukaenda kulipia?!
 
Back
Top Bottom