Nimekutana na “my soulmate” nikiwa nimeshaoa

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
978
Reaction score
2,313
Wanasema “ usifunge ndoa asubuhi mana hujui nani utakutana nae jioni” hatimae kwangu jioni imefika na nimekutana na mrembo alieumbwa kwa ajiri yangu.

She is beautiful, hot, real hot. Ni anaendana na mimi yani ile couple ambayo baba na mama wote ni super handsome and beauty.

My current wife is hot but not as my soulmate, i feel sorry for my wife but, I discovered the purpose of life. Time will tell.
 
Aisee nimeishia kucheka tu
 
Ulipomuoa ulikuwa unafahamu kuwa siyo “soulmate” wako? Au ulilazimishwa?

Maana usikute umewehushwa tu na huyo mpya ndo useme soulmate.

Kwani nini kinafanya watu wawe “soulmates”?
 
hizo label za 'soulmate' 'other half' na nyinginezo ni uongo mtupu wa kwenye filamu watu wanajidanganyia

umeamua kuoa/kuolewa na mtu, umeingia kwenye makubaliano, unatakiwa uzingatie masharti mzee

unachoona wewe ni ile novelty bias, akili ya binadamu ina tabia ya kuona vitu vipya ni bora zaidi, hii hua inaathiri maamuzi
 
Vineno vya kizungu vipo kuhalalisha upumbavu tu.
 
Usimharibie mwenzako maisha kwa tamaa zako
 
Kaa nae uone uzuri unavyoondoka siku zinavyozidi kwenda. Ni mzuri kwasababu yeye sio mke wako.
 
Kuna mjinga mmoja alinisumbua sana nimtafutie mke,nikamtafutia,tukamsafirisha binti wa watu,kafika kule baada ya mwez jamaa ananiambia kapigiwa simu na mwanamke aliekuwa anampenda sana,sasa anashindwa afanyeje

Nilichoka,niliapa kwasasa siwez waanganisha watu katika ndoa,binti wa watu aloteseka mno mpaka nikataman nimrudishe nimuoe mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…