Nimekutana na skin walker usiku wa kuamkia leo. Alikuwa binadamu, akageuka kuwa mbwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay.

Mwanga wa eneo la maegesho tulikiwa mkali, tukiwa umbali wa kama Meta kumi kutoka kwenye gari, tuliona mwanaume mwenye kama urefu wa futi SITA amesismama wima kwenye mlango wa nyuma wa gari yangu.

Wote tukiwa tumemkazia macho, alageuza pozi akawa kainama kama anafunga kamba za viatu, mara akageuka kuwa mbwa, na kutokomea. Wote tukapigwa na mshangao.

Mke wangu akaogopa kabisa hata kuingia kwenye gari, akawa anaogopa hata Sauti za mawimbi ya bahari.

Nikajaribu kumtuliza lakini kiwango chake cha taharuki kikawa juu sana, hadi walinzi ikabidi waje kujua kuna Nini?

Nikawaelezea tukio, wakabisha, wakasema twende kwenye CCTV camera kuangalia footage.

Basi wakaridisha video ya eneo like, na wenyewe wakaona hakika kilichotokea.

Tukajaribu kuomba copy ya kipande hicho cha video tumekataliwa.

Lakini hakika ukistaajabu ya Musa, utayaona ya uncle Firauni.
 
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay...
Huyu ni Jini aka pepo mumekutana nae na hakutaka kuwadhuru wakati huo ni wakati wa majini haswa hapo mulipo karibu na bahari. Hakuwa mchawi bali ni Jini mfanyie maombi au dua mke wako muoga sana .
 
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay...
Story za we bwana sometime Dah oya mzee unazingua
 
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay...
je kiwango cha maji ziwa victoria kilikuwa kinasomekaje!
 
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay...
Siamini hadi nione hiko kipande cha video
 
Back
Top Bottom