Mkata Mtaa
Senior Member
- Jun 10, 2016
- 136
- 142
Wiki iliyopita nilienda kwenye nyumba moja Mikocheni baada ya kusoma kibao nje, hicho kibao nakifahamu maana mwenye kampuni hiyo zamani nilishafanya nae biashara. Nilipiga honi mlinzi akafungua geti, nikaingiza gari. Akafunga geti, nje nikakutana na mswahili nikamuuliza kama wenyeji wapo, akaniambia wapo ndani, kuna nyumba mbili moja kubwa ya ghorafa mbili na nyingine iko nyuma pembeni ya fibre ya kuunganisha, nikaingia umu nyumba ya pembeni, kuingia tu nikakutana uso kwa uso na wachina 3, wanaume 2 msichana 1, wakashtuka, wanaume wakatoka nje, nikamuuliza msichana mtu fulani yupo? hakujibu, akajifanya hajui kingereza wala kiswahili, baadae akaita mwenzake nikamuuliza, tukawa atuelewani ikabidi nitoa business card kumuonyesha, kanimbia jamaa alisharudi kwao,
cha kushangaza mle ndani tulipokuwa ni supermarket kubwa tu, ina vitu vya China na bei zimeandikwa kichina na ila kuna sehemu digit ni kawaida, nikajifanya naangalia vitu na kuzunguka ndani, lakini hapo hapo naangalia licences zilipotundikwa sikuona, Nilivyoona hili supermaket kwa ajili ya wao tu.
Inakuwaje una supermaket geti limefungwa wakati wote, ata nilipoingia mchina mmoja alimfata mlinzi getini nikaona kama anamgombeza kwa kufunguliwa geti. Sijui kama amepewa onyo au kufukuzwa,
Sijui kama mamlaka husika wanajua kama hiyo supermaket ipo na inalipa kodi stahiki na ipo kihalali,
Na kwa nini wafunge geti wakati wowote, na kibao kilichopo nje ambacho mimi nilikisoma nikajua yule jamaa ndio kahami pale ni tofauti na biashara inayofanyika ndani, maana niliwauliza kama biashara yake anasimamia nani wakaniambia hicho kibao kipo tu akijatolewa tu.
Nawasilisha.