Nimekutana na Supermarket ya Wachina mafichoni Dar es Salaam

Mkuu kwanini usitoe ripoti katika mamlaka husika? At least utakuwa umefanya sehemu yako kama mzalendo!
 
Sio mchina, muarabu, mhindi, mzungu wala yeyote yule kila mtu anatakiwa kulipa kodi na kumfichua asielipa kodi kwa kutumia rasilimali zetu ni kitendo cha uzalendo.

Inawezekana sio kufanya biashara tu labda kuna vitu vingine zaidi wanavyojishughulisha navyo. Tafadhali ukiwa kama mzalendo toa taarifa kwenye vyombo husika.
 
Ipo ikitoka Rose garden kuelekea kwa Mwl Nyerere, baada ya kukata kona na kuvuka tuta la pili kuna kibao kimeandikwa Tanzania China Tourist development Ltd, pale karibu palipokuwa na Office ya TCU,
Ipo umo ndani.
 
nlisikia ukifanikisha kumkamata mkwepa kodi TRA wanakujaza mapesa. tumia fulsa hii
 
Unaweza ukaenda ku report sehemu husika ukashangaa unabaki humo kituoni! ukaanza kufuatiliwa wewe! Mbona zipo biashara na makampuni kibao ya kichina biashara zao za kujificha ficha sana halafu ni waoga!
 
Hawana uwoga, waoga ni wahindi, mchina anaogopa kuwekwa ndani wakati ana uwezo wa kulala site anakojenga, wengine wanazibaziba chumba kimoja wanalala wengine wanalala kwenye container, sasa ata ukimweka ndani haoni tofauti kubwa.
 
Ni bora uparipoti.. maana haisaidii kuileta humu halafu ikaishia juujuu.. kwanza je hao wachina wana vibali halali vya kuishi nchini??
Akaripoti wapi? Ndo swali la msingi. Maana anaweza kuwapa watu fursa...hawa jamaa wa mazoezi ya kawaida mtaani wanaweza kwenda kuanza kuchukua mshiko!! Siwaamini hata kidogo.
 
Ipo ikitoka Rose garden kuelekea kwa Mwl Nyerere, baada ya kukata kona na kuvuka tuta la pili kuna kibao kimeandikwa Tanzania China Tourist development Ltd, pale karibu palipokuwa na Office ya TCU,
Ipo umo ndani.
KaMa ni ipo muda mrefu sana nakumbuka mwaka juzi December nikiwa na watching flani nilimpenda ano nikanunia chai za kichina. Wanauza bidhaa zakichina tuu na wapo full. Aisee ni kuwachoma tuu hamna namna. Ngoja niwasiliane na TRA mwenge kesho asubuhi wakakinukishe
 
Sasa we hapo unataka nini mura kwani ujui kuwa hawa ni wasaidizi wa richama retu rire mura
 
Sasa nawe

Wahusika wa Serikali ikisoma hapa iote ilipo hiyo supermarket???

Siungeweka details kamili hapa???
 
Hii style ya kutoa taarifa inapaswa uirudishe kule FB.
Huku JF taarifa hutolewa kwa umakini zaidi, uwazi zaidi na ujasiri zaidi.
Kwa JF hii sio taarifa ni majungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…