Ni jambo la kiutamaduni: Ilitokana na kipindi fulani watu wa ulaya walichukulia wanafalsafa na watu 'ideal' wanakuwaga hawana tamaa tamaa za kimwili sana na ndio maana wakichonga sanamu ya kupigiwa mfano inakuwa na afya njema kimwili, kiakili na kiroho.
So maumbile ndogo kwao inaonesha kujidhibiti na sio 'overindulgance' kwa mambo ya ngonongono.
Lakini kwa utamaduni wa kwetu Afrika kuwa na watoto wengi ni jambo zuri na la kupigiwa mfano, Kuwa baba lao. So kuonesha uwezo kiuzazi ni kitu nzuri tu. Ni utamaduni.
Ni ujumbe fulani, sawasawa na tunavyochorawanasiasa kuwapa midomo na vitambi vikubwa kujaribu kuonesha kitu fulani.