Nimekuwa mtanashati mno, hadi nimekuwa kero kwa wengine

Nimekuwa mtanashati mno, hadi nimekuwa kero kwa wengine

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
7,386
Reaction score
5,965
Wakuu nadhani mko poa,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Nimekuwa mtanashati mno hadi naonekana kero kwa watu wangu wa karibu nini nifanye ili nijiepushe na hali hii.

Kama ujanipata hebu ngoja nikupe mfano wa ninachokieleza, nikisalimiana na mtu kwa kushikana mikono, basi siwezi kuvumilia bila kujifuta na kitambaa au kwa kunawa maji, tena wakati mwingine hata mbele za wale nilioshikana nao mikono kiasi cha kwamba wananiona na wanamaindi na wale wanaonijua huwa hawanipi mikono kwa kuniona kama naringa hivi.
 
Wakuu nadhani mko poa,kama kichwa cha habari kinavyojieleza,nimekuwa mtanashati mno hadi naonekana kero kwa watu wangu wa karibu nini nifanye ili nijiepushe na hali hii ???

Kama ujanipata hebu ngoja nikupe mfano wa ninachokieleza,nikisalimiana na mtu kwa kushikana mikono,basi siwezi kuvumilia bila kujifuta na kitambaa au kwa kunawa maji tena wakati mwingine hata mbele za wale nilioshikana nao mikono kiasi cha kwamba wananiona na wanamaindi na wale wanaonijua huwa hawanipi mikono kwa kuniona kama naringa hivi.
Too much is harmful
 
Kwamba umekuwa Michael Jackson ss na ww wa Tanzania's
 
Kwamba umekuwa Michael Jackson ss na ww wa Tanzania's
Natamani sana niache hii tabia lakini nashindwa kabisa,kwa mfano nikimpakia mtu kwenye mkweche wangu basi akishuka nitapafuta sana pale alipokaa tena nashindwa hata kuvumilia nifike mbali ndio nifute,sasa unakuta hata yule niliyempakia anakuwa hajafika mbali.
 
Una dharau halafu uliishi maisha ya shida sana huko nyuma ndio maana ulivyopata ukajiona mtu fulani wa ajabu ungeenda kuishi mwenzini basi....ulimbukeni nyie ndo mnakanaga wazazi kisa hawana mionekano mizuri ...
 
Hata mimi nitakumaind tusalimiane halafu unawe mikono mbele yangu.
 
Use this formular to solve your problem.....


293047.image13.png
 
Hizo ni DALILI mbaya sana kijana...umelelewa ki SINGLE MAMA? Fuata ushauri wa wanaume wenzako mapema sana kabla hujaanza kujiskia miwasho ktk washeli
 
Back
Top Bottom