Nimekuwa mtu napenda chai kupita kiwango

Mr C Kauli huru

Senior Member
Joined
Nov 26, 2023
Posts
148
Reaction score
199
Naombeni kuuliza kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu

Nimekuwa napenda kunywa chai kila muda ninapokula chakula iwe mchana au usiku. Nahitaji kila nikila chakula basi na kikombe chachai pembeni pasina kujalisha ni chakula gani.
Wakati mwingine nahitaji tu kuinywa yenyewe

Swali langu ni je kunywa chai sana hakuna madhara kiafya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mtu wa kanda ya Kaskazini? Preferably Arusha na Kilimanjaro. Wale watu wanakunywa sana chai.

Unywaji wa chai una faida lukuki. Ila pia una athari zake.

Tuanze na athari za unywaji wa chai;
1. Unywaji wa chai wakati wa kula, unazuia sana ufyonzaji wa madini chuma. Na hivyo kupelekea upungufu wa damu mwilini. Haishauriwi sana kwa walio na upungufu wa damu kutumia chai ya rangi wakati wa kula.

2. Majani ya chai yana kiwango fulani cha caffeine. Hivyo utumiaji wa mara kwa mara wa chai kunaweza kusababisha kukosa usingizi, moyo kwenda mbio, nk.

3. Chai inahitaji sukari. Na watu wengine huweka kiwango kikubwa sana cha sukari hivyo huweza kuleta uzito mkubwa na pengine kisukari.

Faida za kunywa chai;
1. Kuchangamsha mwili. Kule Arusha na Kilimanjaro, wenyeji wakiamka lazima wapige chai. Kuondoa ile baridi na kufanya mwili uwe active.

2. Inasaidia sana kwenye mmeng'enyo. Chai ikiwekwa tangawizi, inasaidia katika ufyozaji w madini katika vyakula. Hii huleta afya njema.

3. Chai pia ni kimiminika.
Sasa inasaidia mwili kuwa na kiwango kizuri cha maji. Watu waanaokunywa chai sana ni nadra kusikia kiu na mwili kuishiwa maji (dehydration).

4. Kuna research kadhaa zilifanyika na kuonesha chai inasaidia katika kupunguza uzito. Haswa utumiaji wa green tea na pia kuweka kiwango stahiki cha Cholesterol.
 
Kauraibu hako.
Kumbuka kuzidisha kila kitu kuna madhara unaweza usiyaone sasa
 
Wewe ni mtu wa kanda ya Kaskazini? Preferably Arusha na Kilimanjaro. Wale watu wanakunywa sana chai.

Unywaji wa chai una faida lukuki. Ila pia una atharo zake.

Tuanze na athari za unywaji wa chai;
1. Unywaji wa chai wakati wa kula, unazuia sana ufyonzaji wa madini chuma. Na hivyo kupelekea upungufu wa damu mwilini. Haishauriwi sana kwa walio na upungufu wa damu kutumia chai ya rangi wakati wa kula.

2. Majani ya chai yana kiwango fulani cha caffeine. Hivyo utumiaji wa mara kwa mara wa chai kunaweza kusababisha kukosa usingizi, moyo kwenda mbio, nk.

3. Chai inahitaji sukari. Na watu wengine huweka kiwango kikubwa sana cha sukari hivyo huweza kuleta uzito mkubwa na pengine kisukari.

Faida za kunywa chai;
1. Kuchangamsha mwili. Kule Arusha na Kilimanjaro, wenyeji wakiamka lazima wapige chai. Kuondoa ile baridi na kufanya mwili uwe active.

2. Inasaidia sana kwenye mmeng'enyo. Chai ikiwekwa tangawizi, inasaidia katika ufyozaji w madini katika vyakula. Hii huleta afya njema.

3. Chai pia ni kimiminika.
Sasa inasaidia mwili kuwa na kiwango kizuri cha maji. Watu waanaokunywa chai sana ni nadra kusikia kiu na mwili kuishiwa maji (dehydration).

4. Kuna research kadhaa zilifanyika na kuonesha chai inasaidia katika kupunguza uzito. Haswa utumiaji wa green tea na pia kuweka kiwango stahiki cha Cholesterol.
Hasante mkuu umenijibu ipasavyo. Na wala hujakosea niko Arusha na natokea Kilimanjaro. Haliyahewa nayo huchangia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chukua izi

1. kila kitu kikizidi kina madhara.

2. usiuendekeze mwili mara eti mwili wangu umezoea hivi au unataka vile

3. wewe ndo uukontroo mwili na sio mwili ndo uanze kukukontroo wewe.

4. kunywa ivo vyai kwa kiasi mkuu.
 
Naombeni kuuliza kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu

Nimekuwa napenda kunywa chai kila muda ninapokula chakula iwe mchana au usiku. Nahitaji kila nikila chakula basi na kikombe chachai pembeni pasina kujalisha ni chakula gani.
Wakati mwingine nahitaji tu kuinywa yenyewe

Swali langu ni je kunywa chai sana hakuna madhara kiafya?

Sent using Jamii Forums mobile app
KARIBU KISUKARI NA CHUNVI KUONDOKA
 
Hiyo siyo kauli japo unahaki yakiuandishi humu. Ungejua kisukar kinavyotesa hakika tungejua jinsi ya kukiepuka kwa 100% tungekiepuka ila mengine nikwa mkono wa Bwanatu. Usimtamkie mtu hivyo mkuu tushauriane tujuzane tujue kipi nikip mazingira hutufundisha vitu vingi sana tofauti tofauti vyahaki na dhalimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe umeanza kupenda chai mkuu?

Chai inanoga uzeeni...

With experience.
Mimi kitambo tu napenda kunywa sana chai na Wala mimi sio mzee ndio maana nimekubishia ila kwasababu ya experience si kupingi maana ni kweli atamimi Huwa nawaona wazee wanapenda kunywa chai ama kahawa au Tangawizi
 
Ngoja tukupe na shamba la chai kabisa..

Ili uendelee kunywa..[emoji508][emoji508]
JamiiForums68569125.jpg
 
Back
Top Bottom