Wewe ni mtu wa kanda ya Kaskazini? Preferably Arusha na Kilimanjaro. Wale watu wanakunywa sana chai.
Unywaji wa chai una faida lukuki. Ila pia una atharo zake.
Tuanze na athari za unywaji wa chai;
1. Unywaji wa chai wakati wa kula, unazuia sana ufyonzaji wa madini chuma. Na hivyo kupelekea upungufu wa damu mwilini. Haishauriwi sana kwa walio na upungufu wa damu kutumia chai ya rangi wakati wa kula.
2. Majani ya chai yana kiwango fulani cha caffeine. Hivyo utumiaji wa mara kwa mara wa chai kunaweza kusababisha kukosa usingizi, moyo kwenda mbio, nk.
3. Chai inahitaji sukari. Na watu wengine huweka kiwango kikubwa sana cha sukari hivyo huweza kuleta uzito mkubwa na pengine kisukari.
Faida za kunywa chai;
1. Kuchangamsha mwili. Kule Arusha na Kilimanjaro, wenyeji wakiamka lazima wapige chai. Kuondoa ile baridi na kufanya mwili uwe active.
2. Inasaidia sana kwenye mmeng'enyo. Chai ikiwekwa tangawizi, inasaidia katika ufyozaji w madini katika vyakula. Hii huleta afya njema.
3. Chai pia ni kimiminika.
Sasa inasaidia mwili kuwa na kiwango kizuri cha maji. Watu waanaokunywa chai sana ni nadra kusikia kiu na mwili kuishiwa maji (dehydration).
4. Kuna research kadhaa zilifanyika na kuonesha chai inasaidia katika kupunguza uzito. Haswa utumiaji wa green tea na pia kuweka kiwango stahiki cha Cholesterol.