puker hizi hali si wewe pekeyako unapitia.. Kila mmoja katika hatua ya makuzi, utu uzima ama uzeeni hupitia changamoto zinazofanana na zako ama nginginezo.. Tunachotofautiana ni nyakati, vipindi na uzito
Umefika mahali pa kujikataa na kukata tamaa .. Hii ni mbaya sana.. Kamwe usipoteze tumaini kwakuwa hakuna gumu lisilo na mwisho..
Kuna miaka na vipindi vigumu sana tunapitia kwenye maisha.. Ambao hawakuwa imara walijidhuru kwa vilevi nk na wengine walijimaliza
Katika nyakati hizi mshike sana Mungu wako kwa imani yako.. Sali sana fanya sana ibada.. Kuna nguvu kubwa kwenye sala na ibada.. Muombe sana Mungu akuvushe salaam lakini kubwa kuliko yote muombe akupe mwisho mwema!
Una nafasi ya kuingia JF na kuandika. Una simu una bundle una mikono.. Kuna wengine hawana vyote hivyo
Maisha ni fumbo gumu na majibu yake yako kwenye utulivu na ukimya na sala
Don't give up buddy.. For in the darkest hour of life there is always a twinkle of light to lead you through...
Nakuombea....!!!