Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Kwa Africa mwanamke kutembea na mume wa mtu siyo kesi kesi na ni hatari mwanaume kutembea na mke wa mtu
Kumbeeee....ni kwamba wanawake wnalenda kushare 🍆🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mnawapaga vitu gani wanaume wenzetu maboya ao husikute hata wazaz wake kijiji wanaishi maisha duni wadogo zake Kula Yao nishida
Wala sio maboya, kila mmoja ana uwezo wake wa kuhonga!
 
Ukimuacha kiajabu ajabu unaweza kwenda mbinguni bila kutarajia.tiketi nzuri ya kusafiria anga na usirudi tena duniani ni mapenzi kwa sasa.chomoka bila hata kumgusa.kuwa makini kakugharamia huyo na amefanya ivyo akijua wewe ni wake tu ili usiende sehemu nyingine na wala usitamani cha mtu.that y amekugharamia hivyo.
Fanya hivi mpeleleze mkewe mchonganishe na mkewe .ili mkewe afanye amekugundua wewe mchepuko.kama atakuwa na nguvu huyo mke mwenzio atatakiwa kuchagua wewe au yeye.
Kama ni muislaam itakuwa imekula kwako utakuwa mke wa pili
La sivyo baada ya uwo ugomvi utajidai umekimbia vurugu za mkewe nawe unakuwa unaliungurumisha na huyo mkewe jamaa atachoka ugomvi itabidi akuache
 
Dada tunaomba update!

NB: hilo penzi jipya litakuponza, nina mifano miwili ya waliokimbilia true love na kuacha mme wa mtu....wamepaukaje sasa in the pursuit ya kuitwa Mrs , lol wanajutaa

Soon
 
Yani mtu anakupenda, anakuhudumia, amekubadilishia life, yuko proud na wewe.

Umuache kisa ili uwe na mahusiano na kijana.

Ambaye naye atakuchekupukia tu.

Anyways, I'm kinda polygamous.
As naendelea kukua naelewa tu ndoa, titles za mahusiano and all along that line havina uhusiano wa moja kwa moja na aina ya mahusiano one shud have.

Hapa sana sna nakushangaa tu.
Ukikua utanielewa.

Hahaaa
 
Ukimuacha kiajabu ajabu unaweza kwenda mbinguni bila kutarajia.tiketi nzuri ya kusafiria anga na usirudi tena duniani ni mapenzi kwa sasa.chomoka bila hata kumgusa.kuwa makini kakugharamia huyo na amefanya ivyo akijua wewe ni wake tu ili usiende sehemu nyingine na wala usitamani cha mtu.that y amekugharamia hivyo.
Fanya hivi mpeleleze mkewe mchonganishe na mkewe .ili mkewe afanye amekugundua wewe mchepuko.kama atakuwa na nguvu huyo mke mwenzio atatakiwa kuchagua wewe au yeye.
Kama ni muislaam itakuwa imekula kwako utakuwa mke wa pili
La sivyo baada ya uwo ugomvi utajidai umekimbia vurugu za mkewe nawe unakuwa unaliungurumisha na huyo mkewe jamaa atachoka ugomvi itabidi akuache

Cant take that chance. Soon naleta updates of what i did.
 
Naandiks kwa herufi kubwa DADA SIKU ZA MWANaDAMU KUISHI NI CHACHE TUBU MAANA UNAKARIBIA KUFA
Ujue mtu akiwa anakaribia kufa anawqshwa washwa kama wewe sahiz [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona simple tu. Mrudishie gari. Mrudishie nyumba. Anza upya tu na huyo bwege wako ndio utakapokuja kujua kwamba kumbe ulikuwa unamuacha ksbb tayari amekupa ujanja mjini. Ukajua utaendelea kuwa navyo hata usipokuwa nae
Kuna ndugu yangu alimuacha mwanaume ambaye alikuwa anampa kila kitu pamoja na kumhudumia mtoto wake mwenye ulemavu. Si akapata kijana mwingine. Akaachana na yule baba na kuolewa na huyo kijana. Sasa hivi anajuta na ile ndoa kule imekufa na yule kijana wameshaachana. Kumbe yule kijana alipendea hela ambazo alikuwa anapewa na huyo baba. Yule baba ni muislam alikuwa na mpango wa kumuoa kama mke wa pili. Yule baba saizi kaoa mke wake mwingine kamnunulia gari na nyumba safi. Yule dada yuko tu anadanga na majuba yake
 
Ikifka muda wa kutaka tuachane,hakikisha kuwa unanirudishia gharama zangu zote,kuanzia kodi,mavazi na nyumba niliyokujengea!

Maisha magumu yanawapeleka vibaya,shida zikiisha mnaanza kutaman kutoka!

Nakusubiria leo unikabidhi TUACHANE!

NIKO SERIOUS
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.

Pia soma: Mrejesho: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo
Huna akili
 
Back
Top Bottom