Nimekuwa nikikumbwa na usingizi mzito wakati wa vikao na wakati nikiwa katika nyumba za ibada. Shida yangu nini?

Nimekuwa nikikumbwa na usingizi mzito wakati wa vikao na wakati nikiwa katika nyumba za ibada. Shida yangu nini?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari wadau wa JF.

Kwa miaka takriban minne sasa, napitia nyakati ngumu. Nikiwa kwenye vikao mbalimbali vya kijamii, kikazi au hata Imani napatwa na usingizi wa ghafula.

Pia niwpo ktk nyumba ya ibada, mawaidha na mahubiri yakiendelea najikuta nimesinzia tena usingizi mzito. Ninapata muda mwingi wa kulala na kazi zangu sio nzito.

Kuna kikao fulani mwaka juzi nilisinzia hadi mwisho nashutuka, kikao kinafungwa.

Je, tatizo langu ni nini?
 
Umetupiwa mapepo ya kukufarakanisha na bosi wako.

Katikati ya kikao unakoroma, boss wako anakutazama tu, unachafua hewa ukiwa usingizini, tena kwa sauti ya juu, boss wako anakutazama tu.

Tu udenda tunakuchirizika, boss wako anakutazama tuu, yaani kifuatacho sasa, Mungu aepushie mbali, muombe sana akunusuru na usingizi huo mzito
 
Kwanza weka mwili wako fiti yaani upunguze unene ila kama uko fiti basi jua kuna shida either hupati muda sahihi wa kulala au una shetani linakusumbua. Kusinzia katika nyumba ya ibada huletwa na Shetani.
 
Umetupiwa mapepo ya kukufarakanisha na bosi wako.
Katikati ya kikao unakoroma, boss wako anakutazama tu, unachafua hewa ukiwa usingizini, tena kwa sauti ya juu, boss wako anakutazama tu.
Tu udenda tunakuchirizika, boss wako anakutazama tuu.... yaani kifuatacho sasa, Mungu aepushie mbali, muombe sana akunusuru na usingizi huo mzito
Hilo la miaka minne iliyopita limenigharimu tayari. Aliyekaa pembeni yangu hata hakuniamsha kwa kunigusa tu.
 
Kwanza weka mwili wako fiti yaani upunguze unene ila kama uko fiti basi jua kuna shida either hupati muda sahihi wa kulala au una shetani linakusumbua. Kusinzia katika nyumba ya ibada huletwa na Shetani.
Mimi mwembamba, pia nafanya mazoezi
 
Mimi mwembamba, pia nafanya mazoezi
Mzee basi hiyo itakuwa ni Sihr (uchawi)...either umeambatana na shetani au umelishwa . Jaribu sana kumuomba Mungu akuondoshee matatizo hayo lakini pia kama una nafasi tembelea katika maduka ya dawa za asili ulizia dawa inaitwa habbat sawdah ( black seeds) nunua pakiti ya mbegu zake zilizosagwa kisha changanya na asali unywe atleast vijiko vitatu daily, pia nunua na mafuta yake ...uwe unajipaka eneo la paji la uso na pembeni ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu.

Pia unaweza kutafuta vitunguu swaum...vipondeponde kisha kabla ya kulala jipake usoni na kwenye mishipa ya fahamu kichwani. Mungu atakufanyia upesi uweze kuondokana na tatizo hilo.
 
Jaribu kutumia tiba ya vitunguu swaum na Ndimu kama una sheytwan basi ataondoka kwa uwezo wa Mungu ktika mwili wako.

Nunua kitunguj swaum kimenye punje zake kisha kisage vizuri halafu chukua ndimu kama tatu hivi kamulia then mixture yake utaitumia kujipaka mwili mzima usiku kabla ya kulala. Kama unaweza unaweza kupaka na asubuhi siku ambazo huendi kazini. Kama una matatizo ya kuvamiwa na majini wachafu basi yataondoka kwa uwezo wa Mungu
 
Back
Top Bottom