SoC01 Nimekuwa volkano

SoC01 Nimekuwa volkano

Stories of Change - 2021 Competition

Kitumba_

Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
30
Reaction score
21
Mlima ni moja kati ya sehemu zinazovutia kutazama, haswa kama unatazama kwa mara yako ya kwanza. Lakini kama ulishawahi kuuona mlima fulani au milima kadhaa, kwa namna ambayo inaitwa karibu kila siku, hata mlima unakua tu ni moja ya sehemu za mandhari. Yaani Mlima... ni mlima...ni mlima tu.

Hapa nipo. Mlima mwingine.

Sio kihivyo, nimekua VOLKANO!.

Pale ambapo mlima unakuwa VOLKANO, unabadilika unakua hai! Unatoa mwanga juu! Unaangaza mwanga! Kuna kuwa na kitu kinatokea! Unakua mtu!

Sasa, Nimekuwa VOLKANO!

Usiwe tu sehemu ya mazingira. Au kuwa tu sehemu ya mkusanyiko fulani. Au mshiriki tu wa kikundi fulani. Au mmoja wa waajiriwa mahala fulani.

Kuwa mtu fulani 'spesho'. Kama VOLKANO!. Watu wanaweka umakini kwenye VOLKANO. Ni mlima fulani unaovutia, na kama unataka watu wawe makini nawewe basi kuanzia sasa niige Mimi. Kuwa jeshi la mtu mmoja linalovutia!. Kuwa macho, uwepo wako uonekane,Tingisha na sogea. To a mwangaza! Kiundai ungua hasa uzalishe joto ambapo kwa nje utatoa mwangaza, kuwa kitu fulani hivi! Yaishi maisha yako vile unataka, kuwa mtu fulani!

Watu wanaheshimu VOLKANO! rahisi tu ni kwasababu ya moto sana kushika, VOLKANO inafanya mengi zaidi ya mwali wa moto. Joto lake linasambaa sana, unayeyuka, ile lava ina moto mwekundu mno unasambaa kutokea katikati. Hakuna cha kuzuia, mtu au chochote kile kitakacho jaribu kusimama kwenye njia yake. Ni moja ya ushahidi wa kiasili kuhusu nguvu ya Muumba! hivyo watu wanaheshimu.

Unahitaji kuteka 'attention'?
Unahitaji kuipata heshima?
Unahitaji kuwa usiozuilika?

Basi, kuwa Mwanadamu VOLKANO!.

Na hakikisha unakumbuka chanzo cha nguvu ya volkano... JOTO kwo pata MOTO!!!.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom