Nimelazwa hapa MOI,kiherehere na ushamba wangu ndio umenifikisha hapa

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Long story short,baada ya kufika kwenye mlango wa hizi benki moja za kisasa nikawa natumia nguvu nyingi sana kufungua mlango,kumbe nilivyokuwa nafanya sivyo ,yaani unatakiwa ukikaribia mlango wewe endelea kutembea tu mlango unasense kuna mtu then unajifungua wenyewe,washkaj na mademu waliokuwa karibu walinicheka sana mara "yaani nyie wasukuma tokea ndg yenu awe mkuu mnajidai mnajua kila kitu" nilifadhaika sana nikawasamehe.
Wanasema fool me once shame on you,Ilipofika muda wa kutoka niliulenga mlango vizuri halafu nikafumba macho nakutembea kwa spidi ya hatari ,kumbe kitu nilichokuwa sijui ni kuwa umeme ulikuwa umekatika na wateja wote wanatumia mlango mwingine,nimekuja kushtuka niko MOI.
Dokta ananiambia hapa shingo imeteguka na ninahitajika kufungwa POP ya shingo,maombi yenu tafadhali.
 
hhahahaaa.... apo ukiwa na sandarusi la hela utaona mpaka branch manager atakavyokufuta jasho! ooh sorry, ooh pole darling! pyuuu kumbe wamechungulia upako wa hela....
 
Pole itakuwa hujaumia sana maana umeweza hata kutuma hii thread😀😀
 
Hahaha me ushamba uliniponza na vile vioo kwa nje unajiona kumbe watu walio ndani wanakuchora!basi kila siku nikienda pale benk nachana nywele pale nje najiweka fresh kuchomekea nini maana kulikuwa na mtoto mkali pale namzengea.siku ya siku nimefika akanipa live jinsi nnavyofanyaga pale huku wanacheka na mwenzie kisha wakagonga halo haloo niliona noma
 
Hahahahaaa. Aibu kilo kumi
 
Msaga Sumu hebu acha kutuumiza matumbo kwa kucheka
 
Wanaume wa Dar bwana.. Inamana Huna Ndugu Wa Kuwaambia Unakuja JF..

Ushatangqza na FB if u have a Heart Type Amem?? Na Insta Je ushaweka Picha
 
Ha ha mmepanda hadhi siku hizi kina ngosha! Zamani wasukuma walikuwa wanaficha kabila zao kia utayemgusa utasikia …mi mnyamwezi wa ipuli
 
hahahahahahahaha yan nimecheka kwa nguvu daaah pole sana lakin hahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…