Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,263
Reaction score
3,897
Ndugu zangu wana jamiiforums habari za asubuhi hii ? kwangu mimi ni mzima wa afya na nipo sawa kabisa

Sina cha kupoteza Kama mnavyoona hapo juu kwenye bandiko.

Jana jioni mida ya saa moja nikiwa kazini kwangu kuna dada ninayemfahamu kwa sura tunaishi mtaa mmoja alikuja kazini kwangu, hapo kazini kulikua na watu kadhaa wakipata huduma,

Baada ya watu wote kuondoka alinifata huyo dada akanieleza kwa uchungu mkubwa kuwa "mke wako anatembea na mme wangu mwambie mkeo aachane na mme wangu" maneno hayo aliyatamka kwa kuyarudiarudia na mpaka machozi yakamtoka

Kuna watu wakatokea pale kupata huduma yule dada akaondoka sikupata nafasi ya kuzungumza nae kiundani ili kujua mke wangu alitembea na mme wake lini, na nimeshindwa kuchukua hatua yoyote mpaka sasa nashindwa nianzie wapi, inavyoonekana mpaka dada huyu kulia kwa uchungu mbele yangu itakuwa kweli mke wangu anatoka kweli na mmewake

Ndugu zangu hili suala ni zito kweli kwangu nianzie wapi, majibu sina. Nimeamua kulileta hapa mimi kijana mwenzenu mnipe mawazo nifanye nini nimetuliza akili yangu sijakurupuka ila hatua ya kwanza nimeona nililete hapa.


Asanteni
Yuda_exalioth
Jamiiforums_Geita
 
Umeambiwa mke wako anatembea na mume wa mtu. Aliyekuambia ndiye mtu wa kukupa ushahidi kama anao. Yawezekana ana picha, msg au kitu chochote kama ushahidi. Sasa unapokuja kuuliza humu jf wakati mtu sahihi wa kukuambia ukweli unaye mtaani kwako sijui ukweli upi unaotaka
 
1..kuongea huku akilia kwa uchungu haimaanishi kuwa maneno yake ni kweli kwa asilimia 100,..hivyo hupaswi kuyaamini bila ushahidi....

2..uhusiano wako na mkeo ukoje mpaka sasa?..anzia hapo

3.. ikiwa ni kweli, je unazani ni nini chanzo na nini utafanya?.. swali hili lakupasa ujiulize na ujijibu wewe mwenyewe ukiwa na akili timamu bila stress wala presha ili upate jibu sahihi...

4.. kumbuka NGUVU SIO TIBA BALI HEKIMA NI DAWA....
 
Rudia kusoma wewe
 
fanya mpango wewe na mkeo mkutane na huyo dada akiwa na mume wake at neutral point, uulize upate kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…