Nimelima alizeti zimesombwa na mvua heka 20

shamle

Member
Joined
May 10, 2014
Posts
24
Reaction score
4
Kweli kilimo ni kamari lakini sikati tamaa bado tapambana mpaka kieleweke.
 
kweli kilimo ni kamari lakini sikati tamaa bado tapambana mpaka kieleweke

Wazungu wanamsemo: "When the going gets tough, the tough gets going"!

Mwanamuziki maarufu wa Marekani alicheza Sinema
inayoitwa "Get Rich or Die Trying"!

Kama mafanikio yangekuwa yanakuja kirahisi bila changamoto, nyingine zikiwa nzito za kukatisha tamaa, hakyanani nisingekuwa naposti kwenye uzi huu muda huu!

Piga moyo konde, jipange, rudimo tena na mtumainie Mungu!
 
Mkuu usikate tamaa,
mwaka juzi nilifuga kuku kwa juhudi nakufanikiwa kuwa na kuku 65 lakini walikufa wote
mwaka janaa nikafuga wakafa wote,
na mwaka huu nafuga kwa mara ya tatu,
nikichemka nabadilisha mradi.
 
Mkuu usikate tamaa,
mwaka juzi nilifuga kuku kwa juhudi nakufanikiwa kuwa na kuku 65 lakini walikufa wote
mwaka janaa nikafuga wakafa wote,
na mwaka huu nafuga kwa mara ya tatu,
nikichemka nabadilisha mradi.

Kweli kabisa mkuu, nilifuga kuku wa kienyeji kama 400 hivi wakafa wote, nikarudia tena kama 250 wakafa wote, sasa hivi ninao kama 17 naendelea kupambana! Hakuna kukata tamaa mkuu.....ila kila hatua nimejifunza mambo mengi ya muhimu na yananisaidia sana.Kuku wangu hawa 17 matetea kumi na tatu na wote wanataga sasa na wengine wanatamia mmoja ametotoa kifaranga kimoja na kimekufa, ila nimejua tatizo lilikuwa nini, ni kupambana kwenda mbele....na mbuzi tisa wawili wamezaa wiki iliyopita...naendelea kujifunza...tusikate tamaa na tumtegemee mwenyezi Mungu, kwa hakika tutafika!
 

pole sana mkuu,
badilisha mbinu za mapambano. usikate tamaa usiku unapo komaa kupambazuka kunakaribia.
 
Uzuri kama una nia ya kusonga mbele pale unapokosea unapata somo la kubadilisha mbinu za kilimo. Songa mbele huku ukiamwa una badilisha mbinu
 
kondoa MZEE

Ni kwenye zile mbuga nini? Nina jamaa yangu hapa kwa Mkoloni, naye alilima mitaa hiyo hiyo, ikaja mvua ikasafisha kila kitu,akabadilisha location. Kama ni zile mbuga kwa mafuriko ya hovyo ndio kwenyewe.
 
nashukuru wakulima wenzangu kwa kunipa moyo

Sasa ndio umeanza ujasiriamali hasa, nilikuwa na mbuzi 70 mwaka juzi, siku moja jioni walirudi 36,tena waliorudi ni wadogo wadogo tu. Likawa bonge la somo na nikajua nilikosea wapi, kiujumla kosa lilikuwa langu mwenyewe. Nimerekebisha sasa.

Kama hujakata tamaa, angalia location salama ili mafuriko yasisombe tena.
 
Ni kwenye zile mbuga nini? Nina jamaa yangu hapa kwa Mkoloni, naye alilima mitaa hiyo hiyo, ikaja mvua ikasafisha kila kitu,akabadilisha location. Kama ni zile mbuga kwa mafuriko ya hovyo ndio kwenyewe.

Hiyo mbuga limeni mpunga! Mazao yanayoathiriwa na maji ni pata-potea! Pia mnaweza anzisha kilimo cha dengu, mafuriko yakikata mwezi Wa nne mnapiga dengu! Yasipokuwapo unaponea kwenye hiyo alizeti! Niliishi Kasulu tukakuta raia mbuga hawazitumii tukawafundisha KILIMO cha mpunga, sasa hivi Kasulu inawika kwa KILIMO cha mpunga! Wasukuma hoyeeeeeeee!
 
Kilimo chema kipo njiani utafanikiwa...pole lakini usichoke !! Good luck shamle
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…