Nimelima alizeti zimesombwa na mvua heka 20


nataka kulima dengu mwezi wa nne
 
kweli kilimo ni kamari lakini sikati tamaa bado tapambana mpaka kieleweke

Mimi mwaka Jana nimelima vitunguu eka sita (6) nimetumia milion Tisa (9) nikatoka na laki sita sijakata tamaa saivi nina eka mbili nasubiri baraka za mungu mwezi wa pili katikati kwenye mavuno hivyo pia na wewe nakushauri usikate tamaa maana mpaka nilitaka kujuta lakini nikakumbuka kuwa mungu alipa mtihani ule sijui kwanini maana nilitaka ninunue gari na hiyo hela huenda labda ingeniua sijui naomba ndugu zangu tukumbuke kuwa kukata tamaa ni dhambi tupambaneni mpaka kieleweke
 
next time use insurance, i am flabbergasted at how careless people are with their investments.

pole sana.

Sio suala la Kuwait "careless", Mkuu Mzungu! Unafahamu ni karaha kiasi gani na rushwa kiasi gani inayodaiwa kwa Mwenye Bima hadi alipwe fidia hapa Tanzania? Unafahamu inagharimu kiasi gani kufuatia fidia hadi ilipwe? Ni Shirika gani la Bima Mashambani kama sio wote wamerundikana kwenye Mijini kwenye Viyoyozi tu!
I have nothing against Insurance and a person Insuring his/her properties/products. The issue is, Insurance in Tanzania is a farce!
 
kweli kilimo ni kamari lakini sikati tamaa bado tapambana mpaka kieleweke

Haya yalinikuta mwaka jana, nililima ekari 30 kabla sijapanda shamba likawa na mgogoro zikaenda ekari 22 nikabakiwa na ekari 8, nikapanda mahindi ile yanaanza kuota tu shamba likajaa maji kilichobaki ni maumivu tu. sijui nani aliimba nikabaki nalia na mola.
 

maafisa wa bima kuwa kero sio sababu ya wewe kutoku-insure mazao yako.

Tujifunze kuwa responsible, kama tunataka kweli kupambana kwenye karne ya 21.
 

Kiongozi nami ni mkulima nilikuwa nategemea kupata kiasi kama 20m baada ya kilimo lakini nikapata 2.5m. Unajua yule kibarua aliniita kwa upole akaniambia hivi boss unafikiri Mungu mjinga akupe wewe mil 20 msimu wa kwanza tu wa mavuno? Anataka uitolee jasho kwanza ili uwe na akili ya kuitumia vizuri huku ukiendelea kumtukuza
 
kweli kilimo ni kamari lakini sikati tamaa bado tapambana mpaka kieleweke

Sio kamali kaka. Kilimo kina kanuni zake kama biashara nyinginezo. Namaanisha unatakiwa kuwa na plan yako ya kilimo ikijumuisha pia risks na changamoto unahisi zinaweza kutokea na njia za kuweza kukabili. Nilichojifunza mimi mara nyingi tunasahau kuconsider hali ya hewa katikia mipango yetu ( mvua, temperature n.k).

Kwasasa kaa chini jiulize ni changamoto zipi umepata na utatatuaje.

Thanks
 

asante kwa ushauri
 

Ushauri kama huu sio. Milioni tisa si ndogo ati. Mi nilidhani unamshauri abadili mfumo lakini wewe unamshauri asikate tamaa kwa kutumia mfumo uleule afu ategemee matokeo tofauti! Thubutuuu! Kilimo kina kanuni zake bwana.
Hii mambo ya kubahatisha huku tukijipa moyo wa kutoka ndio imetufkisha hapa tulipo watanzania. Umaskini mpaka basi!
 
Mkuu kila kukicha mambo hubadilika na pia zaidi juhudi na kumtegemea mungu Kwa mtu yeyote mtafutaji hutumia mbinu mbalimbali hasa pale anapoona mafanikio ni madogo au mabaya katika njia anayoitumia wakati uliopo hivyo huwezi kutoa fomula ya utafutaji wakati hujafanikiwa ni hatakama umefanikiwa si wote wanfanikiwa Kwa moja
 
maafisa wa bima kuwa kero sio sababu ya wewe kutoku-insure mazao yako.

Tujifunze kuwa responsible, kama tunataka kweli kupambana kwenye karne ya 21.

That's good thing, Mkuu nipe kaelimu kidogo, kuinsure mazao kuna utofauti wowote na kuinsure magali or nyumba!? Kampuni gani ni nzuri kwa hii aina ya insurance.

Sorry kwa kuchukua muda wako
 
next time use insurance, i am flabbergasted at how careless people are with their investments.

pole sana.

I like this idea, can you share insurance companies which insurers agricultural undertakings. It will help many.
 

Labda pia tunatakiwa tuingie kwenye kilimo chenye kutumia technologia ya kisasa kama umwagiliaji, greenhouses, mbegu bora zenye uhakika wa matokeo mazuri, vifaa vya kisasa nk.
 
Ndio changamoto za kilimo,msimu mwingine lima kisasa na si kienyeji,fuata kanuni za kilimo bora.
 
That's good thing, Mkuu nipe kaelimu kidogo, kuinsure mazao kuna utofauti wowote na kuinsure magali or nyumba!? Kampuni gani ni nzuri kwa hii aina ya insurance.

Sorry kwa kuchukua muda wako


Hakuna shaka, check na NICO

NICO TZ::Welcome to NICO Tanzania

Fanya tafiti kwa makampuni mengine pia.Kama unafahamiana na watu wanaofanya kazi kwenye large agriculture estates watakuwa wanafahamu zaidi.

Ushauri kwa watanzania, tusiwe waoga wa kujaribu vitu vigeni kwetu. Hivi mnafikiria mtu kama Mohammed enterprises anaweza kulima heka zote za mikonge bila insurance?

Ndio wataku-cost asilimia kadhaa ya investment/faida yako. But we all agree that, it's better to get slightly less than nothing at all.

All the best!
 
I like this idea, can you share insurance companies which insurers agricultural undertakings. It will help many.

Check na NICO

NICO TZ::Welcome to NICO Tanzania

Najisikia kichefuchefu kila nikisikia viongozi wa serikali wakipayuka Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa halafu aslimia 99.9 ya wananchi wake wanakuwa exposed to huge risk bila protection. Ynai nchi tata sana hii.

Kumbuka pia, ili uweze ku-qualify kwenye agriculture based insurance, you will have to practice modern agriculture practices as well as have standardized agriculture management structure. It's not as easy as pie, but if you have decided to do something DO IT WELL, or don't waste your tie doing it at all.

All the best kwenye kilimo.My best Regards.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…