OLESAIDIMU
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 19,139
- 9,562
Mkuu usikate tamaa,
mwaka juzi nilifuga kuku kwa juhudi nakufanikiwa kuwa na kuku 65 lakini walikufa wote
mwaka janaa nikafuga wakafa wote,
na mwaka huu nafuga kwa mara ya tatu,
nikichemka nabadilisha mradi.
Kweli kabisa mkuu, nilifuga kuku wa kienyeji kama 400 hivi wakafa wote, nikarudia tena kama 250 wakafa wote, sasa hivi ninao kama 17 naendelea kupambana! Hakuna kukata tamaa mkuu.....ila kila hatua nimejifunza mambo mengi ya muhimu na yananisaidia sana.Kuku wangu hawa 17 matetea kumi na tatu na wote wanataga sasa na wengine wanatamia mmoja ametotoa kifaranga kimoja na kimekufa, ila nimejua tatizo lilikuwa nini, ni kupambana kwenda mbele....na mbuzi tisa wawili wamezaa wiki iliyopita...naendelea kujifunza...tusikate tamaa na tumtegemee mwenyezi Mungu, kwa hakika tutafika!
daah mkuu pole sana, mimi mwaka jana nililima ekari 22 nilitumia karibu milioni 5 nilichopata ni 2m sijakata tamaa kwa kuwa shamba nilikodi nimeamua kununua langu. hivi mwezi wa tatu naenda kufyeka ekari 200 kwa ajili kulima alizeti na mbaazi kule manyara... hakuna kukata tamaa
Mimi mwaka Jana nimelima vitunguu eka sita (6) nimetumia milion Tisa (9) nikatoka na laki sita sijakata tamaa saivi nina eka mbili nasubiri baraka za mungu mwezi wa pili katikati kwenye mavuno hivyo pia na wewe nakushauri usikate tamaa maana mpaka nilitaka kujuta lakini nikakumbuka kuwa mungu alipa mtihani ule sijui kwanini maana nilitaka ninunue gari na hiyo hela huenda labda ingeniua sijui naomba ndugu zangu tukumbuke kuwa kukata tamaa ni dhambi tupambaneni mpaka kieleweke
Ndugu yangu mkasa wako unafanana na wangu,Mimi nilifanya kwa majaribio ekari mbili,nimetumia kama milioni tatu na nusu,ngoma ime bounce, nimefikiria weee nkaona ngoja nijaribu tena,japo nadhani kufuga vitu kama mbuzi ukiwa na eneo la kutosha ni more sure,kuliko kulima!!!