Nimelipia chumba mpaka sasa napigwa chenga!!!! Msaada wenu tafadhali

Nimelipia chumba mpaka sasa napigwa chenga!!!! Msaada wenu tafadhali

shadownet

Senior Member
Joined
Aug 4, 2015
Posts
133
Reaction score
677
Wakuu natumaini wazima, mimi ni kijana ambaye nlikuwa natafuta chumba cha mtaani (ghetto), kwa bahati nlikiona chumba ambacho pana mtu nayefahamiana naye alikuwa kapangisha hapo na ndio alikuwa anataka ahame, aliniambia nimpe pesa ya miezi 6 sawa na 300,000 ili aweze kuongea na mzee wa nyumba anifanyie process nihamie hapo, hio hela nilimpa mwezi wa 10 ila hadi leo huyu mtu anapiga chenga tu, nilifatilia kwa mzee wa nyumba kama alilipa lakini mzee akanihakikishia kwamba chumba hakijalipiwa mpaka sasa, wakuu naombeni msaada wa kisheria nianzie wapi niende wapi ili kukabiliana na utapeli niliofanyiwa na huyu mtu,,ushahidi nilionao ni mpesa nliyomtumia hela, message, na pia hata mzee wa nyumba aweza kuwa shahidi..\

Naimbeni msaada wenu wadau nikabiliane na hili swala kisheria
 
Mliandikishana popote?
Mali bila daftari hupotea bila habari.
 
nenda polisi dogo mchukulie RB MKamate kama unajua alipo na fanya juu chini kesi mmalizane hapo polisi na mkifika mahakamani kama ni mjanja anakuruka na ukaishia kumlipa fidia inahitaji timing kama sio tumia nguvu unamuibukia kibabe mnakunjana mpaka kieleweke au muone sangoma kudadeki ampe kitu inauma mpaka akulipe ,kama vp we piga swala na maombi ya nguvu mungu atende miujiza. mbona atakulhpa tu
 
Back
Top Bottom