Nimelipwa deni langu Tsh. Milioni 1.3 baada ya miezi 6. Nifanye uwekezaji gani?

MUBIKU

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2014
Posts
283
Reaction score
384
Wana jamvi msaada wa mawazo. Kuna sehemu nilidai pesa yangu zaidi ya miezi 6, hatimae leo wamenilipa. Naomba ushauri niifanyie uwekezaji au/ biashara gani ambayo itazalisha na kuongeza thamani ya pesa.

Malipo yenyewe ni madogo tu ni milion1 na laki tatu, eneo nililopo ni Mwanza tayari nimejiwekeza nina nyumba, gari, familia, na kazi ya kudumu.

Ahsante
 
Mtumishi,una nyumba na gari ila hujui namna ya kutumia vijipesa vidogo kama hivyo?

Ok kwakuwa umeomba ushauri acha nikushauri, ingia betpawa kuna mechi ya arsenal na Chelsea ,mpe Chelsea ,ana odd 7 ,hutajuta
Mwenyewe nimeshangaa, mtu mwenye nyumba, gari hawez shindwa manage 1.3M, labda ingekuwa 10M + tungesema saw
 
Wana jamvi msaada wa mawazo. Kuna sehemu nilidai pesa yangu zaidi ya miezi 6, hatimae leo wamenilipa. Naomba ushauri niifanyie uwekezaji au/ biashara gani ambayo itazalisha na kuongeza thamani ya pesa.

Malipo yenyewe ni madogo tu ni milion1 na laki tatu, eneo nililopo ni Mwanza tayari nimejiwekeza nina nyumba, gari, familia, na kazi ya kudumu.

Ahsante
Mh? Mwanza! Kula supu ya sato wanne kila asubuhi kwa siku 7 utapata akili ya nini cha kufanya kama kweli una nyumba, gari, familia na kazi ya kudumu alafu unaona 1.3m kuwa hela nyingi
 
Pole Kwa mikopo ya
Nmb
Crdb
Letshego
Micro credit
Narudia Tena nakupa pole Kwa mshahara usiokepesheka Tena hadi million unateseka hivo fuga kuku au fungua duka la vifaa vya bomba
 
Wana jamvi msaada wa mawazo. Kuna sehemu nilidai pesa yangu zaidi ya miezi 6, hatimae leo wamenilipa. Naomba ushauri niifanyie uwekezaji au/ biashara gani ambayo itazalisha na kuongeza thamani ya pesa.

Malipo yenyewe ni madogo tu ni milion1 na laki tatu, eneo nililopo ni Mwanza tayari nimejiwekeza nina nyumba, gari, familia, na kazi ya kudumu.

Ahsante
Tengeneza Banda la kawaida sana la kuku kama 200 hivi yaani mtafute fundi akupe gharama hiyo!!
Tafuta kuku was kienyeji matetea kama 60 hivi na majogoo kama 10 !!

Nunua dawa kama Newcastle wachanje !halafu tafuta OTC plus dawa ya vitamins!pumba plus chakula special utakua unachanganya na pumba na hicho chakula!!uanze baada ya muda utaanza kuuza mayai ya kuku was kienyeji!mpe hiyo task mkeo !utakua unaongeza kuku wengine pole pole na kuwachanja na kuendelea kufuga kibiashara hasa kuuza mayai tu!!Hela Yako itarudi pole pole!!

Sivyo anzisha duka la chakula kama mchele, maharage dagaa,chumvi mayai,dengu yaani mchanganyiko mama aliuze !!

Jaribu kati ya hizo mbili utakayoona inafaa!!
 
Mtumishi,una nyumba na gari ila hujui namna ya kutumia vijipesa vidogo kama hivyo?

Ok kwakuwa umeomba ushauri acha nikushauri, ingia betpawa kuna mechi ya arsenal na Chelsea ,mpe Chelsea ,ana odd 7 ,hutajuta
Umejuaje ana nyumba na gari?
 
Mimi naona useme uhalisia wako na kazi ulizofanya ndio naweza kukushauri.
Haiwezekani mtu uwe hajawahi kufanya biashara yoyote alafu tukushauri kwa hela ndogo hiyo. Nasema hela ndogo kwa sababu hiyo hela inatakiwa ufanye biashara ya chini ndipo unyanyuke
 
Back
Top Bottom