Nimelipwa deni langu Tsh. Milioni 1.3 baada ya miezi 6. Nifanye uwekezaji gani?

Wana jamvi msaada wa mawazo. Kuna sehemu nilidai pesa yangu zaidi ya miezi 6, hatimae leo wamenilipa. Naomba ushauri niifanyie uwekezaji au/ biashara gani ambayo itazalisha na kuongeza thamani ya pesa.

Malipo yenyewe ni madogo tu ni milion1 na laki tatu, eneo nililopo ni Mwanza tayari nimejiwekeza nina nyumba, gari, familia, na kazi ya kudumu.

Ahsante
fungua genge
 
Tengeneza Banda la kawaida sana la kuku kama 200 hivi yaani mtafute fundi akupe gharama hiyo!!
Tafuta kuku was kienyeji matetea kama 60 hivi na majogoo kama 10 !!

Nunua dawa kama Newcastle wachanje !halafu tafuta OTC plus dawa ya vitamins!pumba plus chakula special utakua unachanganya na pumba na hicho chakula!!uanze baada ya muda utaanza kuuza mayai ya kuku was kienyeji!mpe hiyo task mkeo !utakua unaongeza kuku wengine pole pole na kuwachanja na kuendelea kufuga kibiashara hasa kuuza mayai tu!!Hela Yako itarudi pole pole!!

Sivyo anzisha duka la chakula kama mchele, maharage dagaa,chumvi mayai,dengu yaani mchanganyiko mama aliuze !!

Jaribu kati ya hizo mbili utakayoona inafaa!!
Asante mkuu wazo lako nimelifanyia kazi.
 
Wana jamvi msaada wa mawazo. Kuna sehemu nilidai pesa yangu zaidi ya miezi 6, hatimae leo wamenilipa. Naomba ushauri niifanyie uwekezaji au/ biashara gani ambayo itazalisha na kuongeza thamani ya pesa.

Malipo yenyewe ni madogo tu ni milion1 na laki tatu, eneo nililopo ni Mwanza tayari nimejiwekeza nina nyumba, gari, familia, na kazi ya kudumu.

Ahsante
Kopesha tena maana una matumizi nayo
 
Wana jamvi msaada wa mawazo. Kuna sehemu nilidai pesa yangu zaidi ya miezi 6, hatimae leo wamenilipa. Naomba ushauri niifanyie uwekezaji au/ biashara gani ambayo itazalisha na kuongeza thamani ya pesa.

Malipo yenyewe ni madogo tu ni milion1 na laki tatu, eneo nililopo ni Mwanza tayari nimejiwekeza nina nyumba, gari, familia, na kazi ya kudumu.

Ahsante
kama upo Mwanza nakuomba unitafute inbox Kuna mtu yupo Mwanza anaitwa ndg Charles atakuonyesha kitu Cha kufanya Kwa uwekezaji wa pesa kidogo sana
 
Watanzania ni wababaishaji sana. Mtu kauliza ushauri anaanza tena kuulizwa maswali. Hivi angekuja na swali "nisaidieni kupata mil 1.3 ili nianzishe biashara" mngemjibuje ?.
Hela yake kalipwa huko kazini.
Anataka ushauri kama huna usichangie lolote sio sehemu yako.
 
Back
Top Bottom