kanene
Member
- Jan 25, 2012
- 55
- 6
Samahani ndugu wana jf...niliwahi kufanya kazi ya ku-supply vifaa Halmashauri ya wilaya moja hivi. Kwanza malipo yangu yalichelewa sana mpaka ikabidi nianze kutishia kwenda mahakamani. Baada ya kuwa mkali walinilipa. Nilipopeleka cheque benki baada ya benki kuzipokea siku moja baadae niliangalia balance nikakuta kwamba walikua hawajaipost fedha hio kwenye acount yangu. Nilirudi benki kuuliza kulikoni mbona hela siioni ya cheque nilizoingiza jana yake! NILIJIBIWA KUA HAWA WATU WAMEKULIPA KWENYE ACOUNT AMBAYO HAINA FEDHA....hivyo warudishie cheque zao. Nilipokwenda kuonana nao ikiwa ni mweka hazina wa halmashauri hio niliambulia jibu kua nivumilie mpaka baada ya wiki mbili ndio akaunti hio itakua na fedha. saasa wadau naomba ushauri wenu...hundi ninazo je ninaweza kushtaki ili nilipwe?