Nimelipwa hundi hewa.

Nimelipwa hundi hewa.

kanene

Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
55
Reaction score
6
Samahani ndugu wana jf...niliwahi kufanya kazi ya ku-supply vifaa Halmashauri ya wilaya moja hivi. Kwanza malipo yangu yalichelewa sana mpaka ikabidi nianze kutishia kwenda mahakamani. Baada ya kuwa mkali walinilipa. Nilipopeleka cheque benki baada ya benki kuzipokea siku moja baadae niliangalia balance nikakuta kwamba walikua hawajaipost fedha hio kwenye acount yangu. Nilirudi benki kuuliza kulikoni mbona hela siioni ya cheque nilizoingiza jana yake! NILIJIBIWA KUA HAWA WATU WAMEKULIPA KWENYE ACOUNT AMBAYO HAINA FEDHA....hivyo warudishie cheque zao. Nilipokwenda kuonana nao ikiwa ni mweka hazina wa halmashauri hio niliambulia jibu kua nivumilie mpaka baada ya wiki mbili ndio akaunti hio itakua na fedha. saasa wadau naomba ushauri wenu...hundi ninazo je ninaweza kushtaki ili nilipwe?
 
Halmashauri zaina account nyingi wakiona wewe ni msumbufu unawafuatilia sana wanakupaitia cheque ambayo account yake haina kitu.Kama hujatoa kitu kidogo watakusumbua mpaka ukate tamaa.
 
Wamekulipa kupitia acount ipi? Hata hivyo vumilia ila inabidi uwe mjanja sana kila siku nenda benk wakiingiza uchukue chapu make nako ukichelewa wanaweza wakaingiza then zikachukuliwa na wengine ukaendelea kusota!
 
Serikali huwa wasumbufu kulipa ingawa watakulipa lakini utakuwa umesumbuka,nilishaifanyia kazi halmashauri moja nikawa nawadai mill 42,hadi kulipwa it took a year tena baada ya kusumbuana,kuna jamaa yangu huu ni mwaka wa tatu mpaka wamepelekana mahakamani,kama capital yako ni ndogo usijaribu kufanya nao coz watakuweka juu ya mawe,kuna ambazo ni nzuri kufanya na watu hao kama za kukusanya ushuru wa mahotel,masoko,stand etc ambapo pesa yako unaikata juu kwa juu
 
Samahani ndugu wana jf...niliwahi kufanya kazi ya ku-supply vifaa Halmashauri ya wilaya moja hivi. Kwanza malipo yangu yalichelewa sana mpaka ikabidi nianze kutishia kwenda mahakamani. Baada ya kuwa mkali walinilipa. Nilipopeleka cheque benki baada ya benki kuzipokea siku moja baadae niliangalia balance nikakuta kwamba walikua hawajaipost fedha hio kwenye acount yangu. Nilirudi benki kuuliza kulikoni mbona hela siioni ya cheque nilizoingiza jana yake! NILIJIBIWA KUA HAWA WATU WAMEKULIPA KWENYE ACOUNT AMBAYO HAINA FEDHA....hivyo warudishie cheque zao. Nilipokwenda kuonana nao ikiwa ni mweka hazina wa halmashauri hio niliambulia jibu kua nivumilie mpaka baada ya wiki mbili ndio akaunti hio itakua na fedha. saasa wadau naomba ushauri wenu...hundi ninazo je ninaweza kushtaki ili nilipwe?

Ndio unaweza kuwashtaki. Ni kosa la jinai kutoa cheki ilihali ukijua account yako haina pesa(insufficient fund) Soma sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 ujue nini cha kufanya kabla ya kwenda polisi if not mistaken unatakiwa uwajulishe walichofanya ni kosa so wakulipe ndani ya siku kumi na nne wakishindwa utaenda polisi na copy ya hiyo cheki. Zaidi wasiliana na mwanasheria aliyeko karibu yako kwa ushauri zaidi
 
Wamekulipa kupitia acount ipi? Hata hivyo vumilia ila inabidi uwe mjanja sana kila siku nenda benk wakiingiza uchukue chapu make nako ukichelewa wanaweza wakaingiza then zikachukuliwa na wengine ukaendelea kusota!
wamenilipa na acount ya GF
 
Serikali huwa wasumbufu kulipa ingawa watakulipa lakini utakuwa umesumbuka,nilishaifanyia kazi halmashauri moja nikawa nawadai mill 42,hadi kulipwa it took a year tena baada ya kusumbuana,kuna jamaa yangu huu ni mwaka wa tatu mpaka wamepelekana mahakamani,kama capital yako ni ndogo usijaribu kufanya nao coz watakuweka juu ya mawe,kuna ambazo ni nzuri kufanya na watu hao kama za kukusanya ushuru wa mahotel,masoko,stand etc ambapo pesa yako unaikata juu kwa juu
Asante sana kwa kunipa mwanga ndugu...nadhani unaelewa hizi kazi za uzabuni ukiwa mchanga mara nyingi unakimbilia kazi tu bila kuangalia namna malipo yatakuaje..nashukuru ssana nazidi kujifunza.
 
Benki walifanya makosa kuipokea pesa bila ya kwanza ku-CheckList hiyo A/c ya General Fund ya Halmashauri.
Benki wanatakiwa waishtaki Halmashauri kwa kuingiza Check hewa au kuipiga faini kwa kuwakata pindi hela ikiingizwa.
Unatakiwa uwashtaki Halmashauri wakulipe kwa kukupa check hewa
Wasiliana na Meneja hiyo Benki pindi wakiingiza hela zao zozote kwenye A/c ya GF wakate za kwako kwanza
 
Back
Top Bottom