Nyambura,pole kwa yote. Inaonekana tayari una uamuzi mkononi ila umeuleta Jf upigwe muhuri. Kama uyo mjeda hujataja hata zuri hata moja na umeuambia umma kuwa anakuchuna,je ni vema kuendelea naye?je ndo ulichokitaka kukiona kwa mwanaume? Je malengo yako yametimia? Dada,unapaswa uishi kwa masharti ya dhamira yako,ukiona moyo umetulia kwa uyo,basi kaa ulipo. Kama unaona unateseka ya nini uendelee kusumbuka?dada fanya uamuzi leo. Hamna atayekushauri muachane wakati unaona anakufaa au mugang'ane wakati unaona anakunyonya. Kama ni wanaume tuko wengi or sorry wako wengi ambao hawajaoa,na wametulia. Jaribu kuangaza pande zote uone je kuna mwenye sifa unazozitafuta? Tatizo la wanawake wengi mna inferiority complex. Ni tatizo kubwa. Dada hujasoma na kuangaika ili uishie matatizoni. Kumbuka pia kuna matokeo ya ulevi,je umeyafikiria?mlevi hufanya kila anachojisikia alaf asubuhi anajuta! Je huko tayari kujuta naye pale atapoona yatokanayo na ulevi yamemletea matatizo makuu? Usiogope,naona unawaza eti 'yapi kwani?' ok,ni kuvunjika,kuibia hadi nguo,kuambukizwa kaswende,kisonono,n.k,kugonga au kugongwa na vyombo vya usafiri. Eti anajiuliza mbona kwenye mchango huu kuna n.k ndo nini? Anyway jihadhari unless kama mmeshaamua kuwa mwili mmoja milele. Tofauti na hapo you still have a chance,to sign or shread a paper. All the best through your decision. Kumbuka, Mme bora utoka kwa Mungu.