Nimemchukia mno Baba Mdogo baada ya kujimilikisha nyumba na eneo la babu

Nimemchukia mno Baba Mdogo baada ya kujimilikisha nyumba na eneo la babu

Kwa ufupi ni kwamba, babu yangu katika pilikapilika za kutafuta alifanikiwa kumiliki eneo ambalo lipo jirani kabisa na barabara ya lami, baada ya kustaafu katika shughuli za kiserikali basi akaamua kuhamia kijijini ambapo alifanikiwa kununua shamba na akajenga..

kule mjini akajenga pia nyumba ya vyumba viwili baada ya ile mwanzo kuchakaa,japo hakufanikiwa kuifanyia finishing..utata ukaanzia pale ba mdogo alipokuja kumuomba babu amalizie hiyo nyumba na atakaa hapo hadi gharama alizotumia kwenye finishing ziishe ndipo ahamie kwake..bila hiyana babu akamkubalia ba mdogo na familia yake wakahamia hapo ila cha kushangaza akaanza kuongeza vyumba vingne bila makubaliano, na mwishowe amegoma kabisa kutoka hapo na anadai ni kwake,..

babu alipofariki mwaka Jana, ding mdogo amegoma kabisa eneo hilo analoishi kujumuishwa kwenye Mali za babu, kiukweli nimekuwa disappointed sana na Tabia ya unyang'anyi na dhuluma aliyoionyesha dingo mdogo..

pamoja na kuwa namiliki viwanja vyangu maeneo mbalimbali na pia nna mijengo yangu binafs nimeshindwa kumsamehe na namchukia yeye pamoja na kizaz chake kwa kitendo cha dhuluma alichofanya..

Ushauri: kama kuna MTU anataraji kuiga Tabia hii, basi jiandae na vita vikali vya kifamilia don't dare (usithubutu).
Babu yako ana watoto wangapi waliotangulia kuondoka kabla yake?
 
1.Eneo ni la baba yake,si lako.
2.Unavichukia vizazi vyake
vimekukosea nini?
Acha mteremko, tafuta vyako.

1.Eneo ni la baba yake,si lako.
2.Unavichukia vizazi vyake
vimekukosea nini?
Acha mteremko, tafuta vyako.
Kati ya Mimi na yeye alieshindwa kununua hata uwanja kwa hela yake akasubiri kupora ardhi kwa nguvu nani anaependa mteremko
 
Mali za babu yako zinakuhusuuu nini kijana wa ovyoooo???? ingekuwa alipewa baba yako sawa.... tafutaa mali zako kama baba ako hakukuachia kituu
 
Wamezaliwa kumi ,.wamebak saba
Usinambie kua wote wamezidiwa ujanja na mmoja.

Kuna mawili hapo, ni urithi au alishampa mwanawe mmoja kwa mapenzi yake kwake kabla hajafa?

Kama alimpa kabla hajafa basi hapo wengine hamna urithi kwenye alichompa mwanae. Kama alikua hajampa na kilibaki "cha babu" kinakua cha urithi kisheria.

Kitanzania kama alivyosema mmoja juu huko, anzeni kutoana roho kwa waganga wa kienyeji, mwisho wa siku waganga wanakua wamekula nyingi kuliko thamani ya hicho kiwanja.
 
Wapo saba kwanini apore,.. Kwa ubabe namna hiyo,..
Kama wapo hao 7, baba mdogo kazingua, kama kapewa na babu kuna uthibitisho wowote?...Kama hakuna hao watoto saba (7) wakienda Mahakamani baba mdogo atatema bungo.
 
Kama wapo hao 7, baba mdogo kazingua, kama kapewa na babu kuna uthibitisho wowote?...Kama hakuna hao watoto saba (7) wakienda Mahakamani baba mdogo atatema bungo.
Kibaya zaidi hakukabidhiwa..na alishaitwa na kuambiwa akatafute sehemu yake ili aepushe ugomvi lakini akaondoka na kususia kikako..na Mimi n mmoja ya wajumbe Siku hiyo
 
Urithi limekua janga kubwa sana hapa nchini vijana wengi wa siku hizi wanawaza urithi tu pasipo kutafuta wao wenyewe.
Kuna familia moja nilikuta wanagombana hadi kupelekana mahakamani kisa mjomba kauza sehemu ya ardhi kwa mfanya biashara wa hizi petrol station.
Mjomba mtu alichukua kama ml 70 ? Kitendo hicho kikawafanya wajomba( watoto wa marehemu dada yake) waje wadai urithi wa mama yao aliefariki.
Mahakamani mjomba wao akawakana mimi hawa siwajui naomba mahakama iwaulize wanatoka ukoo upi na majina yao wanaitwa wakina nani?
Mwisho wa siku mjomba akashinda kesi.
Ndo mnavyo danganyana uko kwenye kahawa .kwamba mahakamani ni mambo rahis rahisi tu hivyo sio
 
Kibaya zaidi hakukabidhiwa..na alishaitwa na kuambiwa akatafute sehemu yake ili aepushe ugomvi lakini akaondoka na kususia kikako..na Mimi n mmoja ya wajumbe Siku hiyo
Wajumbe wakomae!...kama mbwai na iwe!...
 
Kibaya zaidi hakukabidhiwa..na alishaitwa na kuambiwa akatafute sehemu yake ili aepushe ugomvi lakini akaondoka na kususia kikako..na Mimi n mmoja ya wajumbe Siku hiyo
Aliambiwa hivyo na nani?
Babu yako au nduguze
 
Babu harithiwi,. Umeshindwa kurithi alivyoacha baba yako unahangaika na babu? Hatari sana mtafutaji. Nakuhakikishia ukiendelea kujipendekeza ktk familia yao wewe ndo utakuwa wa kwanza kumfata huyo baba yao.
 
Back
Top Bottom