Nimemeza kipande cha toothstick kwa bahati mbaya, nini madhara yake.

Nimemeza kipande cha toothstick kwa bahati mbaya, nini madhara yake.

Wewe ndo ambae ulimeza tunda ya ubiyu au mwingine tena?.....Ila majibu ya humu aisee ukiyasoma huwezi jua kama upo Facebook au kwa great thinker
 
Pole sana ndugu yangu. Kuna mambo kama mawili hivi. Moja inaweza kudhoofishwa na acid ya tumbo na hivyo kutolewa kwa njia ya haja kubwa bila madhara. Pili, inaweza kusababisha pancha kwa utumbo na hivyo kupelekea kupata maumivu makali. Ukihisi hivyo wahi kwa daktari mara moja ili upate ushauri.
 
Mtoto kameza jino wakati wa Kula.
Kuna madhara au atalitoa kwenye haja kubwa?
 
Habari wanajamvi,

Leo baada ya kula chakula cha mchana, nlichukua toothstick na kukikata kipande kikubwa kias na kusafisha meno kwa kutoa mabaki ya chakula yaliyojishikiza kati ya jino na jino,
Nkiwa na wadau napiga story, nliomba maji ya kunywa huku stoothstick ikiwa mdomoni,
Sielewi ikawaje, nmejisahau, nkajikuta nmemeza ile stick kwa maji,
Ghafla nkaisikia imekwama katika koo,
Nkikohoa itoke ikashindikana, nkaagiza ndizi mbivu na kumeza nkaona imepitiliza tumboni,

Naomba kujua madhara ntakayoyapata ama nini natakiwa kufanya kupunguza madhara km yapo.
Baada ya wiki uje hapa utupe uzoefu wako wa kumeza tooth pick, (experience sharing)
 
Wewe ndo ambae ulimeza tunda ya ubiyu au mwingine tena?.....Ila majibu ya humu aisee ukiyasoma huwezi jua kama upo Facebook au kwa great thinker
Ji ujinga ujinga tuu ukute ni lizee zima linajibu hivyo na mtu anaomba ushauri...mi watu wa hivyo huwa nawadharau sana...nawaona hata maisha yao ni ya hovyo hovyo...
 
Mtoto kameza jino wakati wa Kula.
Kuna madhara au atalitoa kwenye haja kubwa?
Atalitoa kwny haja...jino dogo hivyo? Mwanangu alimeza sh 50 akaitoa...Mungu huwa anafanya yake kwny ishu za watoto...meza ww mkubwa sasa
 
Back
Top Bottom