Nimemfuma mke wangu akiiba nyama jikoni

Nimemfuma mke wangu akiiba nyama jikoni

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,788
Reaction score
3,033
Leo wife kanikera mno.
Leo nimetoka zangu kwenye miangaiko nikasema ngoja ninunue kanusu kilo kakula na familia.
Mimi nikafika zangu nyumbani nikakabidhi mboga kwa wife nkamwambia andaa msiso.
Nikaenda zangu kuoga bafu ya nje nikatumia tuu dakika chache nikatoka ile namwangalia wife kama alikua anaficha kitu nikamwambia vipi sasa sijui alikua anabuguia na maskini akakabwa tena akaanza kupaliwa mwishowe akatema ile nyama.

Mimi sikupenda kumbana sana nisije kumuaibisha mbele ya watoto nikaamua anifate chumbani nikaammwambia kulikoni vipi.

Akaanza kuona ona aibu na et ooh ulinishtukia ghafla nikaoga mimi tuu nlikua naonja!
Sasa nikamwambia kama unaonja mbona ulikua na wasiwasi sasa hujiamini?
Nikaona nisizozane nae sana nkamwambia wewe ndio mama mwenye mji jiachie kwa raha zako na mimi ni mumeo basi akashukuru akaendelea kwenda kupika.

My take: Nyie wanawake nini kimewakumba? mbona mnakuwa waroho hivi wa nyama?
Acheni hii tabia kama kuna wengine wanaofanya humu mnawafunza wenenu udokozi.

Pia muwe na amani muwapo na wandani wenu bwana acheni kufanya mambo ya ajabu.
 
Alikuwa anakuwekea limpwata....."*"""""*wewe
 
na umwambie mkeo kwamba hicho kitendo kimekukera hadi umeleta huku JF mashemeji zake tujue.
 
Mkuu inaonesha hapo home ni mwendo wa nafaka tu, no samaki, no nyama thats why ameamua kupunguza kiu yake ya nyama jikoni.

My take: jitahidi weka ratba ya nyama even 3 days per week, vinginevyo akitokea jamaa wa bucha(muuza nyama) huyo mkeo ataliwa kirahsi sana.
 
mwaname anahesabu hadi vipande vya nyama ni balaa
 
We ni jipu aisee,yaani inaonekana ni mwanaume mmbeya sana ingekuwa ni mimi ndio mume ningejifanya sijamuona ili asifedheheke.
 
Unatuaibisha wanaume wenzio bana acha ukuda wa kijinga
 
Back
Top Bottom