Nimemfuma mke wangu akiiba nyama jikoni

Nimemfuma mke wangu akiiba nyama jikoni

mh hakuwa na sababu za kudokoa alikuwa anakula kwani kuna ubaya gani...acha roho mbaya kijana mbona hilo ni jambo la kwaida sana...kwani wewe haijawahi kukukuta hamu ya kula kitu kilichopo jikoni baada ya kuhisi harufu nzuri ya chakula?
 
Leo wife kanikera mno.
Leo nimetoka zangu kwenye miangaiko nikasema ngoja ninunue kanusu kilo kakula na familia.
Mimi nikafika zangu nyumbani nikakabidhi mboga kwa wife nkamwambia andaa msiso.
Nikaenda zangu kuoga bafu ya nje nikatumia tuu dakika chache nikatoka ile namwangalia wife kama alikua anaficha kitu nikamwambia vipi sasa sijui alikua anabuguia na maskini akakabwa tena akaanza kupaliwa mwishowe akatema ile nyama.

Mimi sikupenda kumbana sana nisije kumuaibisha mbele ya watoto nikaamua anifate chumbani nikaammwambia kulikoni vipi.

Akaanza kuona ona aibu na et ooh ulinishtukia ghafla nikaoga mimi tuu nlikua naonja!
Sasa nikamwambia kama unaonja mbona ulikua na wasiwasi sasa hujiamini?
Nikaona nisizozane nae sana nkamwambia wewe ndio mama mwenye mji jiachie kwa raha zako na mimi ni mumeo basi akashukuru akaendelea kwenda kupika.


My take: Nyie wanawake nini kimewakumba? mbona mnakuwa waroho hivi wa nyama?
Acheni hii tabia kama kuna wengine wanaofanya humu mnawafunza wenenu udokozi.

Pia muwe na amani muwapo na wandani wenu bwana acheni kufanya mambo ya ajabu.
Mkeo usimwaibishe yeye ndio mpishi , mpishi atashindweje kuonja kama anapika, hata kama akila kuna shida gani ,mimi sijaipenda lugha yako, umpende mkeo ndugu
 
hivi siku hizi hakuna wafundaji wa ndoa? mwanaume mzima anaweza vp kuleta uzi kama huu kwa wanaume wenzake?
 
Mi nilifikili umemfuma akimg,unya nyama ya kichupi kumbe ya bucha!
 
Mkeo usimwaibishe yeye ndio mpishi , mpishi atashindweje kuonja kama anapika, hata kama akila kuna shida gani ,mimi sijaipenda lugha yako, umpende mkeo ndugu
Ukitaka asidokoe nunua nyama nyingi kila siku mpe apike ale akinai wewe unanunua nusu kwa mwezi? Na kikawaida mwanamke mpe pesa yeye ndio aamue apike nini usimfuatefuate sana
 
Huna mke wewe, kama unae basi unaiaibisha jamii ya wanaume wenye wake.
 
Matatizo ya kula ugali na maharage ndio haya. Wanaume wa mikoani shidaaaa. Mbona sisi tunakula nao chipsi kuku mayai kila siku na wala hatu lalamiki.
 
Umekabidhi mboga kwa waifu ukaenda kuoga bafu la uani. Umetumia dakika chache tu kutoka unamkuta waifu amefutika nyama mdomoni. Hio mboga itakuwa hata imewiva japo kidogo kweli?
 
Mkuu mke kudokoa mboga tu unatoka povu hivyoo, na kwa siku hiyoo upo na umeshinda nyumbani umeona hivyoo, waache waonjee

Kwa halii hii lazima nipende ujingaaa[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Mkuu inaonesha hapo home ni mwendo wa nafaka tu, no samaki, no nyama thats why ameamua kupunguza kiu yake ya nyama jikoni.

My take: jitahidi weka ratba ya nyama even 3 days per week, vinginevyo akitokea jamaa wa bucha(muuza nyama) huyo mkeo ataliwa kirahsi sana.
exactly, yani inaonyesha hapo home nyama adimu sana kiasi kwamba vipande vya nyama jamaa anahesabu ole wake akute viko shotii
 
Back
Top Bottom