Nimemkamata mwizi wa Taa (balbu) usiku wa leo

Nimemkamata mwizi wa Taa (balbu) usiku wa leo

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,263
Reaction score
3,897
Inashangaza na inaskitisha...

Ilikua ni majira ya usiku saa saba na ushee usinigzi uligoma kabisa nilikuwa naumwa, tumbo lilikuwa linasokota nikatoka nje kuskilizia maumivu, sasa nikiwa nmekaa kwenye maua yaliyostawi niliona kwa jirani yangu taa za nyumba yake zimeanza kuzima moja baada ya nyingine.

Baadae hapo hapo kwa jirani kulikuwa na taa kubwa ameiweka nyuma ya nyumba nikamuona mtu akielekea kuifuata hiyo taa alipofika eneo ilipo huku mimi nausoma mchezo, taa ilikuwa juu zaidi taa ilizima ghafla jamaa alikua ameshikilia ndoo ndogo ambapo akitoa taa anatumbukiza kwenye hiyo ndoo na fimbo ndefu yenye kimduwala juu

Fimbo imefungiwa chupa la maji lililokatwa likawa na shimo hakuna taa inayoruka ina maana taa inasonteshewa fimbo inakandamizwa na kuchekecha kidogo basii taa inakua imetoka inabakia kwenye li chupa

Basi alitoka hapo nikamuona anaelekea kwangu moja kwa moja nyuma ya nyumba nikafuata taratibu amekalia kuangalia taa nikatokea nyuma yake nikamkaba nikamwambia TULIA UTAKUFA akawa mpole akaanza kujitetea, kwanza karibia mtaa mzima ukua giza utafikiri hatuna luku.

Nikachukua tukaongozana kwa jirani nikamuita jirani akaamka akauliza kuna nini usiku huu? Nkamuuliza hauna luku mbona giza, akasema mbona taa za ndani zinawaka labda zitakua zimeungua, nikawambia huyu hapa mwizi wa taa zako.

Jamaa alipigwa vichwa viwili akaulizwa huwa unapeleka wapi alijibu fasta huwa napeleka machimboni nauza bei ndogo, anasema ikijaa ndoo ndogo ninayozunguka nayo mitaani naenda kumimina kwenye ndoo kubwa (diaba) nililolipaki sehemu, aisee tulimpiga tukaongozana akatupeleka lilipo lindoo likubwa, taa zilikua nyingi kwakweli.

Tukaamua tumpeleke police tukiwa njiani kuelekea huko njiani tukawekwa chini ya ulinzi na walinzi wa mitaani tukaelezea mwanzo mwisho wakatuelewa maana kidhibiti alikua nacho mwizi, tulirudi kulala walinzi tukawakabidhi mtu huyo ndio walimpeleka polisi.


Yuda Exalioth
Natumia Jamiiforums
Karibuni Geita.
 
Inashangaza na inaskitisha...

ilikua ni majira ya usku saa saba na ushee usngzi uligoma kabsa nilikua naumwa, tumbo lilikua linasokota nikatoka nnje kuskilizia maumivu, sasa nikiwa nmekaa kwenye maua yaliyo stawi niliona kwa jirani yangu taa za nyumba yake zimeanza kuzima moja baada ya nyngne,

Badae hapo hapo kwa jirani kulikua na taa kubwa ameiweka nyuma ya nyumba nikamuona mtu akielekea kuifuata hiyo taa alipofika eneo ilipo huku mimi nausoma mchezo, taa ilikua juu zaidi taa ilizima gafla jamaa alikua ameshikilia ndoo ndogo ambapo akitoa taa anatumbukiza kwenye hyo ndoo na fimbo ndefu yenye kimduwala juu

fimbo imefungiwa chupa la maji lililokatwa likawa na shimo hakuna taa inayo ruka inamaana taa inasonteshewa fimbo inakandamizwa nakuchekecha kidogo basii taa inakua imetoka inabakia kwenye li chupa

basii alitoka hapo nikamuona anaelekea kwangu moja kwa moja nyuma ya nyumba nikafuata taratibu amekalia kuangalia taa nikatokea nyuma yake nikamkaba nikamwambia TULIA UTAKUFA akawa mpole akaanza kujitetea, kwanza kalibia mtaa mzma ukua giza utafkiri hatuna luku

nikachukua tukaongozana kwa jirani nikamuita jirani akaamka akauliza kunanini usku huu? nkamuuliza hauna luku mbona giza, akasema mbona taa za ndani znawaka labda zitakua zmeungua, nkawambia huyu hapa mwiz wa taa zako

jamaa alipigwa vichwa viwili akaulizwa hua unapeleka wapi alijibu fasta hua napeleka machimboni nauza bei ndogo, anasema ikijaa ndoo ndogo ninayo zunguka nayo mitaani naenda kumimina kwenye ndoo kubwa (diaba) nililo lipaki sehem,, aisee tulimpiga tukaongozana akatupeleka lilipo lindoo likubwa taa zilikua nyingi kwakwel

tukaamua tumpeleke police tukiwa njian kuelekea huko jiani tukawekwa chini ya ulinz na walinz wa mitaani tukaelezea mwanzo mwisho wakatuelewa maana kidhibiti alikuanacho mwzi, tulirudi kulala walinzi tukawakabidhi mtu huyo ndio walimpeleka polisi.


Yuda exalioth
natumia jamiiforums
karbuni geita.
Safiii Sana mkuu!!
Mngempa kipigo heavy halafu ndo mmepeleke huko
 
mngemchoma moto, ataenda 'selo' wiki anarudi

ana advansi na kuanza kuvunja kabisa
 
Back
Top Bottom