watu wanaosikiliza taarabu kwa wanawake naonaga kama mashangingi ya kimalaya yanayotoa mlango wa uwani, huwa nawadharau sana yaani. ila kwa wanaume naaminigi ni mashoga.
Miaka hiyo hakukua na namna. Radio zilikua chache, muziki kwa kiasi kikubwa ulikua ni muziki wa Dansi wa kizazi cha mwisho cha muziki wa dansi( Twanga, Muungano Band, T. O. T band, Tam Tam, Beta Musica, Diamond Musica, Dar Musica, FM Academia/ Musica, kutaja chache)hapo ni baada ya kizazi cha kati cha muziki wa dansi kufa( Vijana Jazz, Washirika, OSS, Bimalee, MCA International nk)
Wakati huo Bongo Flavor ilikua ndo inachipukia na iliwachukua muda mwingi sana muziki wa Bongo Flavor kukubalika. Kwenye hili kongole ziende kwa watu wa mwanzo mwanzo kabisa kama Mh Sugu, Mh Prof Jay, baadae Jay Moe, MwanaFa, AY, Juma Nature, Ins Haroun na Gangwe Mob, Mh Temba, Lady Jay Dee, Sister P, Ray C, Craz GK! Hao walitumia nguvu kubwa sana kulazimisha hadi Bongo Flavor kufika ilipo. Hiyo ni miaka ya angalau 1997-2002! Sote tunakumbuka Girl Friend ( sound track) ya Filam ya jina hilo hilo!
Kwa hiyo, kwa wakati huo, labda kana mdau ulikua mdogo, vyombo vya habari vilipiga sana nyimbo hizo na hakukua na namna utasikiliza tu kama siyo nyumbani basi kwenye daladala( wakati huo Hiace kwa asilimia 99)
Tumetoka mbali sana! Hata hawa wanabongo flavor wa kileo( ambao wamefanikiwa kiukweli, wanatakiwa wawashukuru sana hao wakubwa, wametumia nguvu kubwa sana hadi watu kuwaelewa kuwa nao ni muziki. Those days, Bongo flavor kwa watu wa makamo walichukulia ni uhuni tu na mambo ya ovyo, narudia tumetoka mbali sana