Ukiamua kulea mimba ya mbakaji wako mimi siwezi kuishi na wewe tena kama mume na mke. Nitakuacha niendelee na maisha yangu.

Ooh kama ni hivyo basi mbona atakuwa karahisisha kazi. Nitakachofanya ni kusepa na kusonga mbele na maisha yangu. Yeye hanipi uhai wangu. Nilikuwepo kabla yake na nitakuwepo baada yake.

Hudhani kama atakuja kukukosea tena? Kama hakushindwa kujizuia kukosea mara ya kwanza ni nini kitakachomfanya asikosee safari zijazo? Na kwenye kuchiti hakuna cha eti ulikosea mara moja maana hilo tendo la ngono ukiondoa kubakwa huwaga ni la kupangwa.

Kuna mchakato mzima unaolitangulia. Kuna kupapasana, kuna kuvua au kuvuana nguo, kuna kujiweka sawa katika mtindo mtakaotumia na kadhalika na kadhalika. Sasa hilo mtu unaweza ukaliita ni kosa la bahati mbaya? Abadani asilani, hilo ni kosa la kupangwa.

Ila mwisho wa siku, kilicho muhimu na cha msingi ni uamuzi wa mtu husika. Kama mtu akiamua kumsamehe mwenzake baada ya kutendwa hivyo basi huo ni uamuzi wake na ana haki ya kuamua alivyoamua. Binafsi siwezi kusamehe. Nitakuacha papo hapo pasipo hata na majadiliano. Wanawake wako wengi mno kuendelea kung'ang'ania kubakia na wewe kama vile sina options zingine maishani.