Kama alivyosema George Herbet (mshairi Muingereza:1593-1633):
"Usaliti unakubalika kwani nafsi inahitaji kitu kimoja tu wakati mwili unahitaji vitu vingi".
Mara nyengine wanaume tuko watu wa ajabu. Mfano, mwanamume unaweza kumwachisha mke au mchumba wa mtu, pengine akiwa mja mzito au na watoto, na ukakubali kubeba mizigo hii, na pengine ukajiona mshindi, dume kama wewe hakuna. Lakini ukashindwa kusamehe iwapo mke au mchumba wako atatoka nje, tena sikwambii aje na mimba ya mwengine. Ni yale yale ya mtenda akitendewa.
Back to topic! Kama ikiwa na mimi ni kiwembe, ninaweza kumsamehe kwa usaliti, lakini nitashindwa kumsamehe kwa mimba, kwa sababu moja tu, "hana akili kiasi cha kubaki na mimba mpaka nirejee". Angelipaswa kuwa na tahadhari, na akili.
Kwa hivyo ikitegemea na mazingira, nitamshauri achague: Ama aende kwa baba wa mtoto wake, au akibaki nami mtoto ampeleke kwa baba yake. Na yeye, ikitegemea ni kwa kiwango gani ananipenda naanajuta, ataamua la pili. Lakini kama ataamua la kwanza, atakuwa amefanya vyema kwa yeye na kwa mimi.