Huyu jamaa ni domo zege mbele ya wanawake, hawezi kujieleza feelings zake. Ndio maana ameweza kuishi na mwanamke asiyempenda kwa miaka nane na bado akampa mimba. Hawezi kumueleza asiyempenda kuwa hana mapenzi naye. Pia hawezi kumueleza anayempenda kuwa anampenda, ndiyo maana licha ya kutompenda huyo anayedai hampendi, hadi leo katika umri wa miaka 34 hana mpenzi mwingine, kifupi hana uwezo wa kumpata. Huyo aliyempata most likely alijitongozesha, na inawezekana kuna factor inayowazuia wengine kujitongozesha. Katika hali kama hii, mhusika hana choice zaidi ya kuoa huyu mama. Asipooa huyu ndio basi tena! Namuombea iwe kweli kuwa huyo mama anampenda kweli kama anavyodai, vinginevyo itakuwa maumivu akija gundua kumbe hapendwi na yeye pia alijua tangu mwanzo kuwa hampendi huyo mwanamke. Kama anaamini wanaume wameumbiwa mateso, basi hili nalo lake ahangaike nalo, si kwa kuwa ana huruma sana na huyo mama, bali kiukweli ni kuwa hana la kufanya, yaani hawezi. Angekuwa na la kufanya na angekuwa na uwezo huo angeshafanya hivyo katika hiyo miaka 8, ni kwamba hana jinsi. Namshauri ajikubali na hali yake, kwamba yuko hivyo hawezi zaidi ya hapo, aoe huyo mama akae naye ndiye wa kwake, hakuna ujanja. Namsikitikia jambo moja, wakikorofishana chochote huko mbele ya safari kitu cha kwanza huyo bwana atakumbuka kuwa hakumtaka huyu mama toka mwanzo, na ataweka chuki isiyoisha. Kila kosa lake hata liwe dogo ataliona kubwa sana. Hatamvumilia kwa lolote. Huyu mama atakuwa anaishi kama amevaa koti lenye *****, hatakuwa na amani. Hata ukimwambia unampenda hatakuamini, maana kwa kiwango hicho cha elimu unachosema nina uhakika hata hapa anapitia, na mjadala ameuona, na sababu zako za kumuoa amezisoma. Hapo hajakutana na mawifi vichwa moto, kila kibaya chake watakachokuambia utaamini maana humpendi. Hutamtetea huyo mama kwa lolote. Yaani zile wanazoita pingu za maisha nyie ndo hasa mtakutana nazo, msoto wa ukweli. Hii amani unayojisikia kuikosa sasa hivi, nakuhakikishia hali kama hii itarudi mara kumi! Mimi nimeoa miaka 13, na huwa tunakutana na changamoto za hapa na pale, na hata mke wangu akiniudhi jambo nikikumbuka tu ninavyompenda huwa nasamehe hapohapo. Kuna wakati naweza kuwa nimeudhika jambo lakini nikitafakari nilipokuwa namfukuzia miaka ile, jinsi nilivyokuwa nabembeleza na nilivyofurahi alivyokubali, na mambo mengine mengi mazuri tuliyofurahia pamoja enzi ya uchumba wetu, nikifikiria machache tu ya hayo basi kosa hata wengine walione kubwa mimi naliona dogo sana na kulifuta mara moja. Hutaweza kufanya hivyo kwa mkeo kwa sababu hujawahi kumpenda. Mimi kabila letu ni wabaguzi, ndugu zetu hawakupenda nioe kabila nilikooa, nilipingwa na napingwa hadi leo, yani mke wangu asifanye lolote utasikia tu maneno 'tulisema!'. Lakini kwa kuwa nampenda sana mke wangu yote hayo huwa nayapuuza, na sasa hivi hakuna anayeniambia ujinga wowote. Wewe hutaweza kusimama upande wa mkeo namna hii kwa sababu humpendi. Lakini bado unalazimika kumuoa maana ndiyo hali yako ilivyo. Cha muhimu kwako ni kufanya mazoezi ya kujikubali kama mlemavu wa miguu anavyojikubali na kuona kusota kwa mikono ndiyo njia pekee ya kumwezesha kutembea, wewe jikubali na hali yako hiyo na changamoto zake ndizo hizo nilizokutajia baadhi tu.