Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Humpendi analazimisha nini! Atimuke zake huko atafute wanaume wengine. Wako wanaume kibao aje kukuganda hapo nini. Kama ningekuwa ni mie asingejaribu hata kutia guu lake mlangoni kwangu. Kosa ulilofanya ni kumtia mimba. Mtoto chukua ukalee.
 
sifikirii kumtelekeza mtoto lakini pia sifikirii kumuoa mama yake mbaya zaidi sihitaji kuwa na watoto wa mama tofauti.

Haya ya mwisho umesema mtoto wake....ina maana huna imani kama ni wako?.
Wewe unaonekana sio mtu wa msimamo na kigeugeu. Kama umeweza kukaa nae miaka mitano huko unainjoy reli ya kati tena inawezekana ulikuwa unampigia simu mwenyewe njoo leo sasa leo unatafuta ushauri hapa wa nini? Kwani ulikuwa hujui mafuta yanaendesha gari?. Inaonekana kuna mambo hujaweka wazi tukuelewe finguka hapa itakusaidia zaidi.
 
ila na wewe uko weak sijui nisemeje, imekuwaje eti miaka 5 unataka kuachana nae na bado ulikuwa unafaidi mkiwa wote.

Mie naamini kuna kitu unapenda kwake sema hujakaa vizuri kujiangalia wewe juu yake.

hukumuacha miaka yote hiyo na hukuvaa kondomu kujikinga, haya katoa posa kwao.
 
Baba oa, huyo pekee ndiye unayemfaham kwa undan, ikiwa ni pamoja na tabia yake; je kuna gal yeyote ambaye utakuja kuwa naye na kumfaham zaid ya huyo? Oa kk, cku iz kuoa cyo fashen et upongezwe na watu mpe nafac mwanao mtarajiwa ya malez ya baba na mama!
 
Baba oa, huyo pekee ndiye unayemfaham kwa undan, ikiwa ni pamoja na tabia yake; je kuna gal yeyote ambaye utakuja kuwa naye na kumfaham zaid ya huyo? Oa kk, cku iz kuoa cyo fashen et upongezwe na watu mpe nafac mwanao mtarajiwa ya malez ya baba na mama!

Nimekupata sheshejr
 
Wanajamvi!
Nashukuru sana kwa michango yenu mliyotoa, kwa kweli imenijenga kukamilifu na labda niseme tu kuwa nimepata mwanga na hatimaye kufikia uamuzi.

Katika michango yenu, baadhi mlionesha kukerwa na uamuzi wangu wa kuomba ushauri hapa lakini nawahakikishia kuwa ni kupitia ushauri katika michango yenu nasema hiki ntakachokisema hapa. Nisingependa kuona mkiudhika kwa uamuzi wangu hivyo ieleweke kuwa mimi ndiye nabaki kuwa muamuzi wa mwisho hasa inapotokea kuwa pengine utaona ushauri wako labda sikuuzingatia.

Kuna jambo ambalo sikulieleza awali na labda niliseme hapa kuwa suala la kinga dhidi ya maambukizi ya UKIMWI tulikuwa tunalizingatia sana wakati wa mahusiano yetu na ndiyo maana hata wakati tukiwa chuoni tulikuwa tunatabia ya kwenda kupia VVU pamoja ambapo mara kadhaa tulikuwa tunapima Hosp ya Mwananyamala na kituo cha afya cha mwenge. Utokeaji wa ujauzito ni pale aliponihakikishia kuwa hazikuwa "siku za hatari" na kwamba asingeweza kupata ujauzito.

Sasa labda nieleze kuwa NIMEAMUA KUMUOA huyu binti, kwa sababu zifuatazo:-
a). Kuacha kumuoa huyu binti mwenye ujauzito leo ni kitendo cha kibinafsi mno kwani nitakuwa sijazingatia malezi kwa mwanangu mtarajiwa na hali halisi ya huyu mama baada ya kujifungua na ukweli kwamba
atakuwa amepoteza moja ya sifa ambazo pengine wengi wanazitaka (binti kuwa fresh)

b). Ingawa sikuwa na maamuzi ya kuoa kwa sasa hakuna binti (msichana) mwingine ambaye tayari nina mahusiano naye yenye lengo la kuwa mke na mume baadaye.

C). Ukweli kuwa ndiye msichana pekee ninayemfahamu angalau vizuri ikiwamo tabia, mazuri na udhaifu wake (tabia alizokuwa tayari kuzionyesha sijui kama zipo tabia ameficha)

d). Umri pia umesogea na nimezungumza naye amekubali kuwa hatanishinikiza suala la ndoa kwa sasa mpaka hapo nitakapokuwa tayari yaani baada ya kumaliza Masters yangu ingawa katika kipindi hicho
nitakuwa karibu sana na mwanangu.

Sasa labda nikubaliane pia na mchango wa baadhi ya wanajamvi kuwa nijifunze kumpenda.....

Nashukuru kwa wote mliochangia, naomba mjadala uishie hapo. Nitawaalika katika maandalizi ya harusi yangu
 
good boy, nliposoma title, nlijipanga kukushambulia, ila nimependa uamuz wako, good na Mungu awabarik
 
Unachekesha kweli ww yaani humtaki uyo mchuchu then unapenda mtoto!
Sina ushauri broda!
 
Aise pamoja na kwamba umeandika post hii kama conclusion,nimeona nitoe maoni yangu japo kwa kuchelewa. Kwa uzoefu na uelewa wangu NDOA ni kitu cha kudumu na chenye mikiki mikiki mingi. Tabia njema au mazoea pekee haitoshelezi kuifanya i-survive baadhi ya dhoruba za maisha.

MAPENZI na urafiki wa kuridhika ni viungo muhimu katika mahusiano ya aina hii. Kwa maelezo yako ni kwamba huna mapenzi ya dhati kwa huyo binti bali unamuonea huruma na kuepuka kuwa mkatili. Amini nakueleza,hakuna ukatili unaozidi kuwa na partner asiye kufeel,yaani maana nzima ya ndoa ndo inavurugikaga hapo na kufanya kila mmoja wenu kuishi kwa mateso ya kukosa penzi la dhati. Better azae, mlee mtoto, umwache huru atafute wa kufanana naye nawe pia kadhalika.

Believe me utakuwa umetenda haki sana kwa kumweleza ukweli kwamba humpendi kiasi cha kuwa mke,ingawa itamuuma na atakuona adui kwa muda lakini kama ana hekima atakuja kukushukuru baadae as compared to lifetime of a loveless relation!
 
"Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo"

Kosa lako liko hapo mkuu. Ulikuwa unajua kwamba huna furaha kwenye huu uhusiano na bado unachapa kavu.

Mimba haitokei kwa bahati mbaya acha kusema bahati mbaya, una elimu ya kutosha kujua mbegu za mwanamke na mwanamme zikukutana kuna uwezekano wa kupatikana mtoto.

Miaka 34 wewe ni mtu mzima, kwahio man up and takecare of that baby and the mother.

Happy Father's day in advance.
 
Ngoja ukome, mtu humpendi bado waenda pekupeku!

Itabidi umwoe kama hutaki watoto wa mama tofauti na akizaa tu ndipo utagundua kumbo mtoto ni wa kihindi!
hahahahahaha!
 
habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi University) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.

Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia kama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.

Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.

Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?


kwa ushauri zaidi soma maneno ya rangi nyekundu hapo juu!
 
"Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo"

Kosa lako liko hapo mkuu. Ulikuwa unajua kwamba huna furaha kwenye huu uhusiano na bado unachapa kavu.

Mimba haitokei kwa bahati mbaya acha kusema bahati mbaya, una elimu ya kutosha kujua mbegu za mwanamke na mwanamme zikukutana kuna uwezekano wa kupatikana mtoto.

Miaka 34 wewe ni mtu mzima, kwahio man up and takecare of that baby and the mother.

Happy Father's day in advance.

Inaonesha uanafahamu vizuri sana juu ya utokeaji wa mimba hasa fertilization process lakini ama kwa makusudi au kusahau hujazingatia ukweli kwamba kuna siku mwanamke hawezi kupata ujauzito hata kama mtashiriki tendo la ndoa mara mia nane kwa siku hizo.

Ninaposema bahati mbaya si kwa kutojua kuwa mbegu za kiume zinaweza kusababisha ujauzito kama kuna yai lipo tayari kurutubishwa bali ni kwa kuwa ulikuwa utokeaji wa kitu ambacho hatukuwa (sikuwa) nimepanga. Na kwa taarifa yako nimeamua sasa kumlea mwanangu (mwanetu) na kumuoa mama yake.
 
Ngoja ukome, mtu humpendi bado waenda pekupeku!

Itabidi umwoe kama hutaki watoto wa mama tofauti na akizaa tu ndipo utagundua kumbo mtoto ni wa kihindi!
hahahahahaha!

Kama ungekuwa umesoma uamuzi wangu kabla ya kutoa ushauri au maneno yako ya kebehi nadhani ungezungumza jambo lingine kabisa. Usikurupuke
 
"Na kwa taarifa yako nimeamua sasa kumlea mwanangu (mwanetu) na kumuoa mama yake"


Hongera sana kwa kufanya maamuzi mazuri na karibu kwenye club (fatherhood) yetu.
 
Back
Top Bottom