Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

I feel you, I feel you!

Angalia usim-spoil, boys are very clever kwa mama zao.

Yuko shule dear, hata kama ningependa nisingeweza! Halafu yeye mwenyewe hapendi, kinajifanya kikubwa na kinatake care of me mostly! "A man of the house" ndivyo anavyojiita!
 
Yuko shule dear, hata kama ningependa nisingeweza! Halafu yeye mwenyewe hapendi, kinajifanya kikubwa na kinatake care of me mostly! "A man of the house" ndivyo anavyojiita!

We kaunga miaka 11 yote hiyo fanya upate mwingine utaumia sana nyonga kwa mtoto wa pili inaweza hata kuleta ukilema mi nilishashuhudia
 
sifikirii kumtelekeza mtoto lakini pia sifikirii kumuoa mama yake mbaya zaidi sihitaji kuwa na watoto wa mama tofauti.

Asee, kwa kuwa umenizidi umri, ila ningekurushia konde through JF. Sasa umeomba ushauri wa nini hapo? Hukuwa ukifikiria haya yote kabla? If you real mean hiyo nyekundu then ifanyie kazi hiyo blue.:angry:

lakini jamaa hampendi....raha ya ndoa kupendana.....mapenzi ya kuoneana huruma hayafai....
kaka mwenye thread.....nakushauri fuata moyo wako.....

Lakini amesema hafikirii kuwa na watoto kwa wamama tofauti, unless aoe anayempenda na wasipate mtoto huko, hapo atakuwa ametimiza Blue na nyekundu hapo juu.
 
Wanajamvi nafuatilia kwa makini kabisa ushauri mnaonipa, nashukuru kwa kuwa baadhi yenu mmenielewa vyema na mnajaribu kuvaa viatu vyangu kabla ya kushauri. Hili naliona vizuri kupitia ushauri mnaonipa though some advices are bitter

Pia naheshimu sana ushauri wa baadhi ya wanajamvi ambao kwao jambo la muhimu kwa sasa ni kulaumu, nadhani hawa kwao ukweli kwamba jambo hili tayari limeshatokea (kwamba tayari mimba ipo) na halizuiliki tena si kipaumbele.

Labda nikiri tu kuwa kupitia uzi huu, hali ya kuchanganyikiwa na kushindwa kujua nini nifanye imepungua na kwakweli napata mwanga. Hapa nakubali kuwa "problem shared lead to problem solved"...

Naheshimu mawazo ya kila mmoja wenu, na naahidi mwishowe nitawashirikisha uamuzi nitakaofikia, bado nafuatilia ushauri mnaonipa
La umenikosha sana mdogo wangu. Nakuomba sana tena sana jitahidi na mwombe Mungu akusaidie kuanza kumpenda huyo dada na mlee mimba hiyo kwa upendo. Mfunge ndoa na kuanza maisha ya pamoja. Hizo hisia za kutompenda zitaondoka ukiamua kwamba sasa moyo wangu naumwaga kwa huyu na utampenda sana umwone wa thamani kwako. Ubarikiwe sana
 
oa baba mtoto wa ujanani huyo jitahidini muongeze fastafasta kabla sperm hazijalegea mthamini kama alivyokuthamini ufaudu vizuri ulichokua ukifaudu.usitake kumtia mwenzio doa kisha umuachie ahangaike nalo jinsi ya kulitoa.nahic umeshanunua tayari na suti ya harusi kamnunulie mwenzio madela
 
Dawa ya penzi ulikuwa uwijui au ulipanga ili uje utuulize?

Cha msingi kubali matokeomsubiri mtoto mlee pamoja
 
Mbona umeshatoa uamuzi ??????

Hutaki mtoto wa nje, na mimba hutoi, Sasa unauliza nini??

Jiandae tu kuishi na huyo mtu wako na utayafurahia maisha bila wasiwasi maana utakua umetimiza ndoto zako za kutokuwa na mtoto wa nje na wala kutoa mimba, \jambo ambalo ni zuri sana
 
sifikirii kumtelekeza mtoto lakini pia sifikirii kumuoa mama yake mbaya zaidi sihitaji kuwa na watoto wa mama tofauti.

sasa unataka usaidiweje? maana kila kitu hufikirii kufanya
 
habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi Univeversity) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.

Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia hama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.

Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.

Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?


athari za NGONO ZEMBE,,,HUMPENDI+KAVUKAVU,,,,
 
Inaelekea binti huyo anakupenda kwa dhati.pili binti anaujauzito wako hivi Mungu unataka akuoneshe nini ili ujue huyo ndio chaguo lako.
Pole kwa mawazo yako finyu ambayo hayana uwezo wa kupambanua mambo kwani we ulivyo ingia kwenye uhusiano ulikuwa unamaana gani licha ya hivyo mlipo kuwa faragha ulisahau kutumia dawa ya penzi.
Sina mengi ya kuandika maana Ndoa umeitaka mwenyewe.



Mimba sio kiashirio cha Upendo!! Hauwezi Kufunga ndoa na Mtu kwa sababu tu unataka watoto wote wazaliwe na Mama Mmoja,au kuogopa kueleweka vibaya na jamii au kuogopa Kuuvunja Moyo Wa Mtu!! Msingi wa Uhusiano wowote ni UPENDO kwa pande zote mbili!! Mtu asijidanganya kama anaweza kuishi na mtu asiyempenda,HAIWEZEKANI,hata kama huyo Mwenza ni Muadilifu na ana Mapenzi kiasi gani,Uhusiano huo Utavunjika tu Mbele ya Safari!!
Hudumia Mtoto na Mama,Lakini yeye aendelee na Maisha yake tu!!
 
lakini jamaa hampendi....raha ya ndoa kupendana.....mapenzi ya kuoneana huruma hayafai....
kaka mwenye thread.....nakushauri fuata moyo wako.....
Preta sikubaliani nawe kabisa. Huwezi k#t*mb@n@ kavukavu na mtu usiyempenda (karne ya VVU k#t*mb@n@ kavukavu ni kipimo cha upendo uliotukuka). Huyo ni muongo wa kutupa. Ingawa mdada baada ya kuona haambiwi suala la ndoa akatumia kanuni yenu, sijui mnaiita PMU. Pia k#t*mb@n@ kavukavu lazima ujiandae na gharama zake. Huyo ngurumbili ya kiume ni mshezi tu wa tabia.

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Preta sikubaliani nawe kabisa. Huwezi k#t*mb@n@ kavukavu na mtu usiyempenda (karne ya VVU k#t*mb@n@ kavukavu ni kipimo cha upendo uliotukuka). Huyo ni muongo wa kutupa. Ingawa mdada baada ya kuona haambiwi suala la ndoa akatumia kanuni yenu, sijui mnaiita PMU. Pia k#t*mb@n@ kavukavu lazima ujiandae na gharama zake. Huyo ngurumbili ya kiume ni mshezi tu wa tabia.

Ndimi Bazazi!

uwiiiiii Bazazi.....umeua ujue.....BTW.....nimekumiss sana......
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom