Wanajamvi nafuatilia kwa makini kabisa ushauri mnaonipa, nashukuru kwa kuwa baadhi yenu mmenielewa vyema na mnajaribu kuvaa viatu vyangu kabla ya kushauri. Hili naliona vizuri kupitia ushauri mnaonipa though some advices are bitter
Pia naheshimu sana ushauri wa baadhi ya wanajamvi ambao kwao jambo la muhimu kwa sasa ni kulaumu, nadhani hawa kwao ukweli kwamba jambo hili tayari limeshatokea (kwamba tayari mimba ipo) na halizuiliki tena si kipaumbele.
Labda nikiri tu kuwa kupitia uzi huu, hali ya kuchanganyikiwa na kushindwa kujua nini nifanye imepungua na kwakweli napata mwanga. Hapa nakubali kuwa "problem shared lead to problem solved"...
Naheshimu mawazo ya kila mmoja wenu, na naahidi mwishowe nitawashirikisha uamuzi nitakaofikia, bado nafuatilia ushauri mnaonipa