Nimempambania kapata kazi, salary ni 1.5m gross kaikataa kisa kapangiwa kwenda mkoani Mbeya

Nimempambania kapata kazi, salary ni 1.5m gross kaikataa kisa kapangiwa kwenda mkoani Mbeya

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
11,931
Reaction score
15,849
Wakuu, naandika hii thread huku nikiwa na hasira za kufa mtu.

Kuna litoto la uncle wangu naishi nalo hapa ghetto, huyu mtu namuona kama sio mzima kichwani kabisa.
Kamaliza Mzumbe na Ka GPA kake ka 4 (nadhani ndio kanampa kiburi)

Alivyomaliza chuo two years back nilimpambania akapata kasehemu ka kujishkiza huko kwenye viwanda vya wachina coz kuna jamaa yangu alinifanyia maneuvers flani wakawa wanampa 500k ambayo haina makato yoyote coz wanamchukulia kama trainee tu.

Well baada ya kuona kila leo anahudhururia Dodoma kupiga paper za utumishi na bado hatoboi nikamshauri aweke nguvu zaidi kwenye private sector kuliko kupoteza resources huko utumishi. So last two weeks kuna mdau wangu mmoja yuko kampuni flani aliniambia ofisini kwao wanataka kijana muaminifu aliyesomea mambo ya kama huyu dogo wangu hivyo nimsaidie kutafuta nikamuambia ninae binamu yangu, tuka arrange kila kitu dogo kafanyiwa interview ya kizushi na akafanikiwa kupita.

So jana wamemtumia offer letter, wamemuambia atareport kwenye office zao zilizopo huko Mbeya na salary ni kama 1.5m gross dogo kasema hayuko tayari kwenda Mbeya kwa mshahara huo labda wambakishe hapa hapa Dar, nimembembeleza dogo naona haelewi, nimewashirikisha wazazi wake naona pia hawajaelewana.

Sasa labda mnisaidie wakuu, huyu mtu mimi nimfanyaje maana pia ananiharibia sifa kwa yule jamaa yangu aliyenipa hii ramani?
 
Huyo umalaya unamsumbua. Anaogopa kumwacha mpenzi wake. Ana akili ndogo za kuona mbali. Siku kibarua kikiota nyasi na mpenzi wake amwambie kuwa ni mjamzito atakuomba tena umpiganie. Hapo ndipo unatakiwa umfukuze kama mbwa akili zimrudie
Sawa sawa mkuu, hawa vijana wetu hawaoni mbali kabisa.
 
Daah! Mitoto ya siku hizi ni ng'ombe kasoro maziwa. Yeye Mbeya anaonaje? Kuna uwezekano hata hajawahi kufika, anakataa tu ksbb ya amepazoea Dar. Lakini Mbeya angee-njoy sana. Ukizingatia ndio anaanza kazi,angefurahia maisha ya Mbeya. Any way achana na huyo mtoto wa mama, yupo mtu anaweza hiyo mkuu nikuunganishe nae, achukue nafasi ya huyo dogo.
 
Back
Top Bottom