Nimempambania kapata kazi, salary ni 1.5m gross kaikataa kisa kapangiwa kwenda mkoani Mbeya

Vyema umetimiza wajibu ongea nae huyo dogo mwambie arudi nyumban kwao akawasaidie wazee wake kazi.
 
HUYO MFUKUZE KARIBU YAKO MAANA IPO SIKU AKIFANIKIWA ATAKUDHARAU HATA WEWE.TUPA KULE, NAJUA UNAJUA KWANINI NIMEANDIKA KWA MAANDISHI MAKUBWA.
 
Kwanza hongera sana kwa Moyo wako huo, usichoke wala mpuuzi mmoja asikubadilishe

Pili, pole sana, naelewa namna ambavyo haya mambo yanavyo dissapoint.

Huyu dogo ndiyo sample ya products za vijana wetu wa kiume wa siku hizi. Maana jauwezi kusikia mambo haya kwa watoto wa kike, labda wawe na altenarnative.

Mbeya ni sehemu ambayo vijana wakienda huwa hawarudi, na kama kuwaondoa basi huwa ni kwa mbinde sana

Kijana hajui akitakacho sababu elimu yake badala ya kumjenga imembomoa
 
Nipo Mimi mkuu ni muaminifu sana
 
Tuliza akili, haufanyi kazi na AI bali huyo ni mwanadamu mwingine mwenye utashi kamili.

Unapomsaidia mtu hata kama amekuomba tambua kwamba hata msaada ubaweza kukataliwa pia. Sio lazima mtu apokee kisa ni msaada.

ANayo maamuzi, yaheshimiwe. Tatizobwatu wengine mnapima thamani ya kitu chochote kwa pesa tu. Kwamba hii ni 5, hii ni 1.5 basi hiyo ni nzuri zaidi. Hapana.

Pia kijana anaweza kuwa hajafikia hatua ya kutoa sadaka kila kitu kwa ajili ya kutunza familia. Muache aenjoi wakati wake. Wakati wake utafika tu.

Nb. Hajakudharau, usimdharau pia. Live and let live
 
Msukume ulingoni akapambane na maisha yenye hasira Kali
 
Mwmbie hiyo GPA kuna wenzake tulipata zaidi ya 4.5 hapo hapo....hivyo isimzuzue.
 
Hii ni fursa mkuu,naomba hii nafasi,mimi niko Mbeya
 
Sema huu uzi wasije watu wakapigwa PM km naanza kupata mashaka kutoka 500k had 1.5M alafu mtu akatae!!! Sio kwa ubaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…