bht
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 10,336
- 1,873
imebidi nianze kusoma kuanzia page ya kwanza ili kupata picha ya nini hasa kimekuwa kukijadiliwa au kuzungumzwa maana leo nilidandia kuanzia page ya 17.
Naweza kusema mambo kadha wa kadha
1: Gs ni (mdada/mkaka) jasiri sana kwa maana pasi kujua kama huyo mkaka/mdada aliyemizmia ni (mke/mume) wa mtu ameelezea namna anavyomfeel. Naomba kumpongeza (mdada/mkaka) aliyepata bahati hii maana naweza sema kwamba ametunukiwa jambo la pekee sana na gs yaani kuambiwa unazimikiwa mbele ya members zaidi ya 17,000 ni jambo la pekee sana.
2: Kwa huyo mdada/mkaka ( namaanisha alyezimikiwa) ningependa awe muwazi kwa gs kama ameoa au ameolewa asije akachukulia hii nafasi adhimu kabisa kumharibia au kum dissappoint gs.
3: Ningependa kumuomba gs akubali matokeo yeyote kama huyo binti/kaka atakuwa ameolowa/ameoa basi lazima akubali kwamba kisicho rizki hakiliki na waendelee kuwa normal friends
4: Mwisho kabisa napenda kusema kwamba idumu jf na mungu awape waanzilishi wake afya tele
huwa siwezi kuiangalia avatar yako lakini kwenye hii post i am able to stand it......