Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumpa mkataba unaoendana na hali yake ni sahihi ila ajue kabla kuwa anasaini nini.Wachezaji wengi wa kigeni wanapokuja Tanzania wanakua wamekaa mda mrefy bila kuwa na timu wengi ni free agent wengine wamekaa miezi sita hawana timu na wengine hata mwaka sasa mtu amekaa mda mrefu bila timu unampaje mkataba mzuri mda mwingine hizi timu zinalaumiwa bure tu
Mayele angekua mchezaji mzuri congo asingekuja Yanga in first place angeenda timu kubwa zaidi ya yanga huo ndo ukweli
Ulitaka nini kitokee baada ya kutolewa? Mashabiki Wakafanye usajili?Kupitia sakata la mayele mashabiki wa simba wameshasahau kwamba wametolewa kombe la FA ni propaganda wanafanya
Kwahiyo alitaka Yanga isimove on?Mayele kinachomuuma ni kusahaulika ghafla Yanga. Ile shangilia yake pia imepotezewa yaani anaona kama kawa ignored completely
Saa nyingine acheni upumbavu, kuna document kibao tunapokea kutoka Uarabuni huwa tunapeleka mpaka Bakwata kutafsiriwa.Kumpa mkataba unaoendana na hali yake ni sahihi ila ajue kabla kuwa anasaini nini.
Umeeleza vizuri sana, japo sijatazama hayo mahojiano lakini kwa maelezo haya, nimeelewa vizuri alichoongea na sababu ya kuongea.Katika mahijiano ya Dakika 50 na sekunde 3 aliyofanyiwa na Azam TV ambayo yameonyeshwa kwenye youtube channel ya kituo hicho, Fiston Mayele ameongea mambo kadhaa, lakini mimi nimeamua kuongelea suala lake la mahusiano na timu aliyoichezea, yaani Yanga pamoja na anayoichezea hivi sasa, yaani Pyramids FC.
Katika mahijiano hayo, Mayele ameonyesha kukerwa na comments za mashabiki wawili au watatu dhidi yake au familia yake na kuamua kuibebesha lawama timu nzima ya Yanga kwa comments za watu hao.
Mayele anasema alipojiunga na Yanga alipewa mkataba na aka sign, ali sign sababu alikuwa hajui kiingereza, Manager wake alikuwa hajui Kiingereza na alikuwa anachekacheka tu.
Ulipoisha msimu wa kwanza, ndipo akasmua kubadili Manager na kumtumia Jasmine ambaye kwanza alishangazwa na ule Mkataba. Akasimamia ubadilishwe, akaongezwa mshahara pia ukampa uhuru wa kuondoka ikitokea club inamhitaji.
Amesema aliahirisha kusema live alichotaka kusema sababu Tanzania ameacha watu wake (familia) ila ameshauriana na Jasmine kwamba mwisho wa msimu ndiyo aongee kila kitu.
Hayo sikuona kuwa ni big issue kivile, kilichonistua na alipoiponda hadi timu aliyoichezea sasa. Mayele anasema alipewa Mkataba na Pyramids FC, mkataba ule Jasmine akaukataa, kwa maelezo yake Mayele akasema “waarabu ni wahuni kama usupotumia akili watakukandamiza”.
Hii kauli inatosha sana kumuweka Mayele katika sintofahamu na maboss wake hao wa sasa.
Mayele anaonekana ni mtu anayependa sana social media na attention zake, siyo mbaya ila, anapaswa kuelewea negative na positive effects za social medias. Hivyo awe mwangalifu sana na aongeacho.
Wana Yanga waliokwazika na Mayele ningewashauri wasiyabebe hayo, ni kijana anajipigania, pia kati ya vitu vinavyopelekea kuwa na kauli zile ni limits aliyo nayo katika uelewa na matumizi ya lugha ya kiswahili. Anajifunza Kiswahili the hardway hali inayompelekea kutoa kauli zinazoonekana kuwa ni kero, kukosa ustaarabu n.k ila yote ni sababu ya kuwa na ufinyu wa uelewa wa lugha anayoitumia, maana anajifunza kurusha ndege huku akiendelea kufanya assembling.
Kama angetumia lugha ya kwao au Kifaransa kamwe asinge strugle. Hivyo muleweni tu na mumuache aendelee na maisha aliyoyachagua.
Mihemko ya nini? Umeshinda njaa siku nzima? Mambo ya kawaida haya, tunajadili kubadilishana mawazo, Upuuzi kwani unatumia hizi hoja kuombea ongezeko la mshahara?Saa nyingine acheni upumbavu, kuna document kibao tunapokea kutoka Uarabuni huwa tunapeleka mpaka Bakwata kutafsiriwa.
Sasa issue ya kutafsiri nayo dunia ya leo ufanyiwe? Huu ni upuuzi sasa.
1. hana busara atapata wapi mawazo ya kipi aongee kipi asiongeeNi ukosefu wa akili huo ma boss Pyramid wakiona hio interview watapata tafasiri gani? sijui kwanini hajui kipi aongee kipi aache
Angerogwq morisson,fei au bangala waliondoka kwa vurugu,mayele kaiingizia pesa Yanga na hata huko aliko ndani ya mkataba wake kuna pesa ya Yanga iwapo atauzwa,mayele mpaka anaondoka Yanga ukiangalia ile documentary ya Yanga alivyoongea akua na ugomvi na Yanga,kikubwa kinachomuuma mayele perhaps alijiona mkubwa kuliko klabu na akajua kuondoka kwake Yanga itayumba,matokeo imekua tofauti na alichokitarajiaPoint kubwa ni kuwa Yanga wanamshambulia Kwa njia za kishirikina...hiyo ndo main point anachojaribu kusema...
Kuna mashabiki anawajua...watu wa ndumba ...wanatumika na club kwenye mambo ya kishirikina...wamekuwa pia wanamshambulia na yeye since aondoke Yanga...
Hiko ndo kilio chake
Mayele hajui Kingereza, lakini Kiswahili anaongea kuliko Mimi.Umeeleza vizuri sana, japo sijatazama hayo mahojiano lakini kwa maelezo haya, nimeelewa vizuri alichoongea na sababu ya kuongea.
Lakini, kubwa zaidi ni ushauri uliotoa ni wa msingi sana. Ni kweli Mayele ana shida ya ujuzi wa Kiswahili, na hii ndiyo sababu ya aina ya kauli zake.
Asamehewe tu.
Ova
Angeweka ushahidi usio na mashaka juu ya hilo.Anaijua Yanga ...keshacheza...na waganga wa Timu anawajua...anawalalamikia kwanini wanataka kumshughulikia kisa kahama Tu Yanga?
Sure mkuu.Angerogwq morisson,fei au bangala waliondoka kwa vurugu,mayele kaiingizia pesa Yanga na hata huko aliko ndani ya mkataba wake kuna pesa ya Yanga iwapo atauzwa,mayele mpaka anaondoka Yanga ukiangalia ile documentary ya Yanga alivyoongea akua na ugomvi na Yanga,kikubwa kinachomuuma mayele perhaps alijiona mkubwa kuliko klabu na akajua kuondoka kwake Yanga itayumba,matokeo imekua tofauti na alichokitarajia