Hiyo rasimu ya Katiba,ni nzuri sana,tunapaswa waTZ wote wanyonge wa nchi hii tumpongeze jaji Warioba na timu yake kwa ujasiri wao mkubwa kwa kuja na rasimu,ambayo ni kinyume cha matakwa ya watawala.
Si mmemsikia Kinana ametamka hadharani kuwa wao CCM hawaiungi mkono rasimu hiyo,hadi wameitisha kikao cha dharula cha CC yao,ambacho kitakutana siku ya Jumatatu.
Lakini waliopigwa na bumbuazi zaidi,ni wale waliokuwa wanausaka urais wa Muungano,kwa udi na uvumba.
Kwa kuwa kwa rasimu hiyo ilivyo hivi sasa ambapo,tutakuwa na Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanzania bara,aka Tanganyika,maana yake ni kuwa marais watakaokuwa na nguvu zaidi ni Rais wa Zanzibar na yule mwenzake wa Tanganyika.
Kwa kuwa rasilimali zote za nchi,kama vile gesi,mafuta,madini ya aina mbali mbali,rasilimali hizo,zitakuwa kwenye wizara za serikali za Zanzibar na Tanganyika,kwa maana hiyo wale.wagombea,waliokuwa wameanza kumwaga mabilioni yao wakiamini mabilioni hayo yatarudi,mara tu wsingiapo Ikulu,kwa namna watakavyofisadi radilimali zetu, wagombea wa design hiyo wajihesabu tu wameliwa,kwa kuwa Rais wa Muungano,baada ya 2015,atakuwa hana tofauti yoyote na malkia Elizabeth wa UK,ambapo nafasi yake ni ceremonial post,mtendaji mkuu wa serilali ya Uingereza ni David Cameron.
Vivyo hivyo ndivyo itakavyotokea kwa TZ,ambapo Urais wa Muungano,utakuwa ceremonial post,nafasi za utendaji na ulaji,zitakuwa ni zile za urais wa Zenj na Bara!!