Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Mchumba hasomeshwi ndg yangu.

Huna haja ya kumtandika risasi ila unaonaje ukamwachia uhai wake ila ukachukua kiungo kimoja ukaishi nacho kikufariji?
 
Achana nae hakuna sheria ya kumlipisha huyo dada. Mcumba hasomeshwi ndugu ulikuwa hujui hili? Hesabu hasara move on. Najua inauma ila ndio uanamme huo
 
Kweli kabisa mkuu hata mimi imenitokea hiyo.mwanamke wa sasa sio wa kumuwekea dhamana ya maisha yako.atakuacha kwa dharau juu
 
Mchumba huwa hasomeshwi aisee, utakufa na presha.
 
Duh! Kuna wanawake wana Royo ngumu jamani!! Yaani unasomeshwa alafu unaruka Kisangani after mafanikio.
Pole sana mkuu cha msingi fuatilia pesa yako iwe fundisho kwao,Kama kweli mliandikishana kisheria.
 
ipo siku atarudi tu, tena kwwa aibu kuu!

Hapo utapata pa kummalizia, maisha ya zunguka kama duara.

Uwe na moyo wa uvumilivu mkuu, hana mdogo wake wa kike umlipizie!😀😡😡
 
'Honesty? Yes, but also, Loyalty an expensive thing you should not expect from cheap people"
Songa mbele
 

Umenena vyema kabisa.

Wakati mwingi kwenye mahusiano ya uchumba Mungu huongea na mhusika kwa kumwonyesha mwenza wake jinsi alivyo na mara nyingi ubaya au udhaifu wake ili ufahamu mapema.

Achana na mambo ya mahakama. Tulizana na umwombe Mungu, utapata mke mzuri utashangaa muda wote ulikuwa wapi.
 
hahahaha mapenzi bana ni sheydaah tupu, hapa home kwangu kuna binti ambae ni rafiki wa mke wangu kaja kusalimia, kapigwa kibuti na mchumba wake aliekuwa amemwahidi kumuoa but kamgeuzia gia angani na kuoa binti mwingne, sasa huyu shem tangu jana analia tu na kuzimia kla akimkumbuka huyo mwenzeke tumempeleka hospital kapima presha iko juu. kazi kweli kweli
 
Alafu kiukweli kweli hapo kwenye kumdai hizo hela mahakamani angepotezea tu kabla hajajiumiza mwenyewe, ebu imajin unamdai hizo hela alafu jamaa wake wa sasa anakuja kuzitoa zote kwako tena kash, itauma sana!!
Mkuu, hata kama mahakama wakikubali hiyo kesi, mwisho wa siku jamaa atakuja kudaiwa RISITI za malipo aliyofanya kwa huyo binti na yeye hana....hatimaye kesi itafutwa kwa kukosa ushahidi. Mkuu hii issue aachane nayo itakuja kumuumiza kichwa bure.
 
tatizo lenu mnawadharau sana wale wanaoandika ujumbe katika guta,pikipiki na malori, wana busara za kiwango cha phd japo hawajaenda shule...walishasema muda mrefu tu...mchumba hasomeshwi
 
Mkuu, hata kama mahakama wakikubali hiyo kesi, mwisho wa siku jamaa atakuja kudaiwa RISITI za malipo aliyofanya kwa huyo binti na yeye hana....hatimaye kesi itafutwa kwa kukosa ushahidi. Mkuu hii issue aachane nayo itakuja kumuumiza kichwa bure.

au amshitaki kwa kumjeruhi kisaikolojia!!!!
 
Nipe nafasi huyo aliyepigwa kibuti maana wafu wanawazika wafu wao
 
potezea km vile uliweka hela kwenye kapu la sadaka ...kwenye kanisa la kiroho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…