Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Pole Sana ila kumbuka Kila binadamu lazima apitie maumivu ya mapenzi ili akili ikae sawa

Sasa ukipitia Hilo hapo tunasema umeiva
 
Pole sana Mdogo wangu , siku zote girlfriend huwa asomeshwi yaan usithubutu kumlipia ada hata ya kodi ya nyumba we muhonge tu tuvi hela vya chips lkn usifanye uwekezaji
 
Mshukuru Mungu kila jambo hutokea kwa kusudi ila ulifanya makosa sana kumwamini mwanadamu. mwamini mke wako ambaye umeshamuoa si vinginevyo.
Hiyo gia kubwa acha kupoteza muda wako Mungu akikuhurumia atakulipia kisasi vinginevyo utazidi kuharibu hata pale ambapo ungetengeneza maana unavyozidi kutafuta kulipiza ukikwama unaweza kujinyonga
 
Uzi wa zamani huu,tulishawafundisha sana,siku hizi nadhani wameacha na ndio maana kesi hizi zimepungua...
 
Ah. Singekubali. Lazima ningempa mimba.

Thredi ya 2016! Sijui iliishaje kwa huyu dogo.

Kusomesha mchumba ni upuuzi. Kama huyo mchumba alimwona anafaa kipindi akiwa chini, afikapo juu huwa na mtazamo tofauti.

Kwa nini kumbeba ‘raw product’ wakati kuna ‘finished and tested products’??
 
Umejidhalilisha zaidi kupeleka shtaka mahakamani. Nashauri kaa kimya. Usimtafute mama yake wala yeye wala ndugu yake.

Unajua Mungu siku zote hakosei. Huyo mwanamke pengine angakuja kuwa tanzi kwako na kukupotezea maisha kabisa. Mshukuru Mungu kuwa kuna kitu amekuepushia huko mbeleni badala ya kulaumu.

Kaa kimya, kama ni mtu wa maombi fanya maombi sana, soma sana neno la Mungu ili Roho wa Mungu akutawale. Najua kipindi kama hiki ndo kipindi ambacho ibilisi huvizia na kumvaa mtu vizuri na unaweza kufanya jambo ambalo utalijutia maisha yako yote. Ukiwa mwenyewe fanya maombi sana na kusoma neno la Mungu usiruhusu nafasi hata kidogo ya ibilisi kuingia ndani yako.

Ukimya wako ndo utamuumiza sana yeye binafsi na familia yake. Ila ukilipiza kisasi tu ndo utakuwa umeharibu kabisa. Mwache aendelee na maisha yake braza. Mbona wanawake wamejaa teleee🙁

Mungu atakulipia yeye mwenyewe na hutaamini kuna siku atakukumbuka tena sana tu na itakuwa too late kuurudisha moyo wako. Jikungute songa mbele boss. Mwanaume wa ukweli hakati tamaaa kirahisi so far una nguvu, u mzima, hajakunyanganya akili yako, maisha yanasonga tuu. Kwani ulizaliwa naye? Mmekutana tu ukubwani.

ONYO: ACHANA NA TABIA KUSOMESHA MWANAMKE ATI AWE MKEO. KAMA UNAMSOMESHA MSAIDIE TU KAMA MSAMARIA MWEMA ILA ACHANA NA MAWAZO YA KUTAKE ADVANTAGE YA KUOA.KAMA ITATOKEA MBELE YA SAFARI POA; ISIPOTOKEA POA!!
Hii imekaa vizuri sana.......neno la Mungu ni chakula tosha cha roho....
 
Sikujua laiti ningejua, najuta.

Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa nimepangiwa kazi mkoa fulani katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu binti nilitokea kumpenda, mzuri kisura na kitabia very innocent niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano ya nyuma.

Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena moyoni kabisa na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo zake ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti yule nilimpenda kutoka moyoni.

Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tushauriane kwasababu kwao nilikua nafahamika. Kwakuwa mimi nilisema nitamuoa binti wakashauri nimsomeshe kama nina nia yakweli. Uwezo wa kumsomesha nilikua nao nikakubaliana na tukaandikishana kwamba namsomesha mimi lakini mwisho wa siku yeye atakuja kuwa mke wangu na hata mahari sintolipa kwani itakua imeingia huko.

Familia ilinishukuru sana kwani waliamini kusoma kwa binti itakua afadhali katika ukombozi wa maisha yao. Binti alikuwepo wakati maandikishano yanafanyika na mashahidi walikuwepo nakumbuka binti alilia yule akiapa kunipenda milele na mapenzi tuliyofanya siku hiyo siwezi kusahau ilikua best sex ever.

Wakuu nifupishe binti alianza chuo kila kitu nililipa nauli hosteli ada matumizi kila kitu ilikua mimi,mwaka wa kwanza ukaisha vizuri mapenzi yanachanua.Likizo naenda likizo zao anakuja, mama mtu alinishukuru sana. Mwaka. Mwaka wa pili matatizo yakaanza nikipiga simu naambiwa yuko library mara assignment nikiuliza zaidi anakua mkali nikasema labda labda kweli shule lakini hata mimi nilisoma muda wa kuongea na mwenzi wangu nilikua nao nikasema labda shule ya sasa ni ngumu. Binti akabadilika majibu ya jeuri nikaenda kuongea na mama yake amkanye naona akajirekebishe na kweli akatulia maisha yakaendelea. Upside zikiwa chache. Mahusiano yalitawaliwa na migororo

Kufupisha Miezi kadhaa imepita binti kaniandikia meseji eti "NAKUSHAURI UTAFUTE MWANAMKE MWINGINE MIMI SIKO TAYARI KUWA NA WEWE NIKUTAKIE MAISHA MEMA"

Naandika huu uzi wakuu acha nikipiga simu haipokelewi mara haipatikani. Nikampigia mama yake kumuuliza kama anajua lolote akasema hafahamu. Nikaomba likizo kazini nifatilie sikuamini siku naambiwa ana mimba na anaishi na mwanaume mwingine. Nilitamani ardhi ipasuke kumbe ndio maana niliandikiwa ule ujumbe nikajiuliza maswali bila majibu,basi angefanya nisijue na mimba juu kapata inauma sana. Kumuuliza mama yake hana analonijibu, kumbe chuo kapostpone sijui anaishi na huyo mwanaume moja ya mitaa Dar, yote hiyo nafatilia kwa baadhi ya marafiki zake na kibaya zaidi huyo mwanaume alishamlipa tena huyo mama pesa nyingine. Na ndio kamchukua binti yake.

Nimechukia kuuziwa mbuzi kwa gunia.Love is blind inakuwaje sikuona yote hayo? Why me..Why.. Najiuliza sipati majibu, sikuwahi kupenda kama nilivyompenda huyo binti. Nilimpenda kutoka moyoni na kujitoa kwake sijawahi kumfanyia mwanamke yoyote niliyomfanyia leo ameniacha kwenye mataa na nyodo juu, kuna muda natamani ningekuwa na bastola nimsambaratishe ila that is not me. Juzi nimeona whatsup kaweka picha yake tumbo kule na namba yake nikafuta.

NILICHOFANYA;

Nimepeleka hii kesi Mahakamani kwasababu tuliandikishana kama mke nimekosa basi nilipwe gharama zangu najua haiwezi kuziba pengo kufuta maumivu naona is the least i can do for my self. Wakuu nifanyaje au nimekosea kupeleka shtaka polisi tumeshaitwa mara mbili hakuna mtu aliyetokea upande wao. Nimetokea kuwachukia wanawake sana. Kwanini mnatufanyia hivi jamani tuwapende vipi. Nimekaa hapa kitandani nimewaza mawazo mengi moyo wangu kama barafu naishia kusononeka.

Sijui nimfanyie kisasi gani aumie kama mimi nilivyoumia.

Adios.

Wanaume wengine vichwa maji..ivi unaanzake kujiwekea eti namsomesha mchumba ili akimaliza awe wangu..Oa endelea kusomesha wewe..na kama huitaji asome unasema mke wangu sitaki usome..cha msingi ongea na mmewe mtarajiwa akurudishie gharama zako..ningekua mimi ningesambaratisha familia nzima..btw haiwezi kuwa mimi sbb sina io akili mgando..au ulirogwa mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Thredi ya 2016! Sijui iliishaje kwa huyu dogo.

Kusomesha mchumba ni upuuzi. Kama huyo mchumba alimwona anafaa kipindi akiwa chini, afikapo juu huwa na mtazamo tofauti.

Kwa nini kumbeba ‘raw product’ wakati kuna ‘finished and tested products’??
Ukute nilishacomment wisdom but ufufuo ukanikuta nimechoka akili na mwili nikiwaza kuzoeana mimba tuuuu.😂😂
 
  • Thanks
Reactions: RR
Watu mnapenda yaani unamsomesha binti eti utakuja kumuoa.?? Kwanza pole afu sheria inaruhusu mtu kudai chake uchumba ukivunjika hivyo dai chako ila kuwa makini usije rogwa kwa maana watu km hao wanakimbilia kuroga hata kukuua. Dai chako sheria ya nchi inaruhusu
 
Mleta Thread Nipo Chini Ya Miguu Yako, Lakini Sikuchungulii
Kama Bado Upo JF Tafadhali Lete Mrejesho Wa Hii Kitu
 
Back
Top Bottom